Jengo la makao makuu la klabu ya Yanga SC, liliopo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam lilivyokuwa linaonekana jioni ya leo baada ya mfululizo wa mvua zinazoendelea nchini. Hali hii imekuwa ya kawaida sasa kwa wakazi wa Jangwani na maeneo mengine ya mabondeni Dar es Salaam wakati wa mvua za masika mafuriko huwakumba, lakini kiangazi hali huwa shwari. Hata hivyo, hali hiyo husababisha athari kubwa ikiwemo vifo vya watu kadhaa na hadi sasa imeripotiwa watu takriban 30 wamepoteza maisha. Poleni Yanga SC, poleni wakazi wa mabondeni kwa ujumla, Mungu awe nanyi katika wakati huu mgumu. Amin, |
0 comments:
Post a Comment