NDANI ya wiki moja, kocha Mreno Jose Mourinho ameshuhudia wachezaji wake mwenyewe wakimuangusha kwa kujifunga mabao ambayo yaliikwamisha timu.
Beki wa England, John Terry alianza kujifunga kwa kichwa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Crystal Palace mwishoni mwa wiki iliyopita, Chelsea ikilala 1-0 na kujipunguza kasi kwenye mbio za ubingwa.
Siku tatu baadaye beki David Luiz akajifunga bao la pili kwa kichwa pia wakati Chelsea ikiwa imefungana 1-1 na PSG katika mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mjini Paris, na mwishowe The Blues ikatepeta zaidi na kulala 3-1.
Mourinho alikasirika, lakini maelezo yake hayakumlenga mchezaji mmoja aliyefanya makosa kwa sababu anajua, soka ni mchezo wa makosa, na hao waliokosea ndiyo ambao kila siku wanamfanya afurahi.
Jana Chelsea imeshinda mabao 3-0 katika Ligi Kuu ya England dhidi ya Stoke City na kurejea rasmi kwenye mbio za ubingwa ikitumia kikosi hiki; Cech; Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Lampard/Luiz dk70, Matic, Willian/Cole 78, Schurrle/Hazard, Salah na Torres.
Unaweza kuona Terry aliyecheza pia dhidi ya PSG jana alirejea kikosini wakati Luiz aliingia kipindi cha pili na bila shaka mchezo ujao dhidi ya PSG ataanza.
Manchester United ilipigwa mabao 4-1 na wapinzani wao wa Jiji, Manchester City Septemba 22, langoni akiwa amesimama kipa David De Gea Quintana na mlinda mlango huyo wa Kispanyola ameendelea kufungwa katika mechi zilizofuata, lakini amebaki kuwa kipa chaguo la kwanza.
Alikuwa akifungwa tangu Sir Alex Ferguson bado kocha Man United, tena mabao mengine rahisi kabisa- lakini amevumiliwa hadi leo.
Yule Petr Cech wa Chelsea mara kadhaa anafungwa mabao rahisi kabisa, lakini ameendelea kuwa kipa chaguo la kwanza The Blues.
Mwanzoni mwa msimu huu, ukuta wa Arsenal ulipewa sifa nyingi kwa kutofungika kwa urahisi- lakini sasa umetepeta na unafungika, tena kwa urahisi mno, ila bado kocha Arsene Wenger hajatoa kashfa kwa mchezaji yeyote na anaendelea kutumia watu wale wale.
Kipa Mpoland, Wojciech Tomasz Szczesny alifungwa mabao sita Arsenal ikichapw 6-3 na Manchester City Desemba 14, mwaka jana, akafungwa mabao matano Arsenal ikifungwa 5-1 na Liverpool Februari 8, akadaka tena na kutunguliwa mara sita Arsenal ikilala 6-0 mbele ya Chelsea Machi 22, mwaka huu.
Lakini huyo ndiye kipa wa kwanza wa Arsenal- na Wenger ana imani naye sana tu, kila baada ya mechi kama atafanya makosa, basi ataambiwa tu namna ya kurekebisha dosari zake, lakini ‘hauliwi’.
Kucheza mpira Ulaya raha sana, unakosea wala husakamwi, inachukuliwa kama kosa la kibinadamu na unapewa fursa ya kurekebisha makosa yako.
Said Mohamed Kasarama alikuwa mmoja wa makipa bora nchini wakati anasajiliwa Yanga SC mwaka 2011 na alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars- lakini kwa kufungwa penalti tatu Yanga SC ikilala 5-0 mbele ya mahasimu, Simba SC Mei 6, mwaka 2012 alifukuziliwa mbali na kupoteza dira yake katika soka.
Shadrack Nsajigwa naye kwa sababu alimkwatua Emmanuel Okwi kusababisha penalti hizo, naye akatupiwa virago pia.
Simba SC iliamua kuachana na kipa Juma Kaseja kwa maelezo kwamba alifungwa bao jepesi katika kipigo cha 2-0 kutoka kwa mahasimu Yanga SC Mei 18, mwaka jana. Lilikuwa bao la kwanza lililofungwa na Didier Kavumbangu kwa kichwa akiunganisha kona.
Yanga SC wakaona watani wao wamekosea kuacha kipa bora, wakamsajili kwa dau la Sh. Milioni 40 mwaka huu, lakini mlinda huyo ameanza kusakamwa pia na huko baada ya kufanya makosa kadhaa yaliyoigharimu timu.
Kevin Yondan alisajiliwa kwa mbwembwe kutoka kwa mahasimu, Simba SC- lakini huwezi amini baada ya kusababisha penalti iliyofanya Mgambo JKT wafunge bao la ushindi dhidi ya Yanga SC Jumapili iliyopita, naye pia anasemwa vibaya.
Sasa najiuliza wachezaji wa Ulaya wanaolipwa fedha nyingi kila siku wanafanya makosa, lakini hawaadhibiwi kwa kiwango cha adhabu za wachezaji wetu huku Tanzania.
Nchini kwetu, fanya vizuri misimu 10 mfululizo, lakini kosa moja tu ndani ya dakika 90 utatamani ardhi ipasuke. Labda huku kwetu soka ni kwa ajili ya malaika tu.

0 comments:
Post a Comment