// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); HAYATOU ASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA NA KUTOA UJUMBE UZITO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE HAYATOU ASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA NA KUTOA UJUMBE UZITO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, April 11, 2014

    HAYATOU ASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA NA KUTOA UJUMBE UZITO

    RAIS wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF),  Issa Hayatou ameungana na watu mashuhuri jijini Kigali, Rwanda kwa ajili kuadhimisha miaka 20 ya Mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda.
    Alitembelea Makumbusho ya Mauaji ya Kimbari ya Kigali, ambako aliweka shada la maua kwenye kaburi la halaiki. Rais Hayatou ambaye pia alikuwa akiwakilisha Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kutokana na nafasi yake Makamu wa Rais wa FIFA", alisema.
    Issa Hayatou katikati katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari mjini Kigali, Rwanda 

    “Soka siku zote litatumika kuwaunganisha watu na kuleta upatanishi. Janga hili halitakiwi kupewa nafasi ya kujirudia katika historia ya binadamu. Soka litaendelea kutumika kama kifaa cha kuwaunganisha watu wa Afrika na litaendelea kuwa kiungo muhimu cha kuunganisha watu na kuzisaidia nchi kujikinga na kupambana na Mauaji ya Kimbari duniani kote.”
    Hayatou aliongeza, “Kilichotokea hapa mwaka 1994, hakitakiwi kuruhusiwa kutokea katika nchi nyingine yoyote, iwe Afrika au ulimwenguni. Sisi kama CAF, tuko hapa kuuonyesha ulimwengu kuwa tunaweza kuungana na kwa kutumia silaha nzito iitwayo soka. soka linanguvu na linamfikia kila mtu; kuweka mabadiliko chanya na maendeleo ya nchi nyingi.”
    Tangu mauaji ya kimbari, Rwanda imepiga hatua kadhaa kwenye soka, kutokana na kuandaa michuano ya Afrika kwa Vijana (Chini ya miaka 20) mwaka 2009, Michuano ya CAF chini ya Miaka 17 mwaka 2011 na watakuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mwaka 2016.
    Rais Hayatou aliongeza kusema kuwa CAF iliwapa Rwanda nafasi ya kuandaa CHAN mwaka 2016, ilikuisaidia nchi hiyo katika mchakato wake wa kuendela kupatana na kutengeneza umoja ndani ya nchi na bara la Afrika linataka kuiunganisha Rwanda wakati ulimwengu ukiangalia vipaji vya Kiafrika vikipambana kwa ajili ya heshima, lakini pia itathibitisha jinsi gani nchi hiyo imeendelea baada ya mauaji ya Kimbari.
    Rais Hayatou aliongozana na Makamu wa Rais wa Pili wa CAF, Almamy Kabele Camara, Katibu Mkuu wa CAF, Hicham El Amrani na Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka la Rwanda, Nzamwita Vincent Degaule.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: HAYATOU ASHIRIKI KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA MAUAJI YA KIMBARI RWANDA NA KUTOA UJUMBE UZITO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top