KOCHA wa Bayern Munich amemshutumu Wayne Rooney kwa kujirusha na kumponza Bastian Schweinsteiger atolewe nje kwa kadi nyekundu usiku wa jana Manchester United wakiweka hai matumaini ya kuendelea na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Schweinsteiger pamoja na mchezaji mwenzake, Javi Martinez wataikosa mechi ya marudiano Jumatano ijayo nchini Ujerumani baada ya Robo Fainali ya kwanza kumalizika kwa sare ya 1-1 jana.
Wakati Schweinsteiger akimnyooshea kidole Rooney aliyekuwa ameanguka chini, kocha wa Bayern, Pep Guardiola alionekana kumuonyesha ishara ya kujirusha refa Mspanyola, Carlos Velasco Carballo na baadaye akasema hajakubaliana na uamuzi huo. "Hapana kabisa," alisema Guardiola.
Ameenda chini: Bastian Schweinsteiger alimchezea rafu Wayne Rooney na kutolewa nje kwa kadi nyekundu
Anaenda chini: Schweinsteiger akimkwatua Rooney
Siyo vizuri babu: Schweinsteiger akimnyooshea kidole Rooney kumtuhumu kujirusha
Sijapenda kabisa: Schweinsteiger akimlalamikia Rooney
"Ni pigo. Hao ni wachezaji muhimu sana kwetu. Tutajaribu kwenda Nusu Fainali, kisha watacheza,".
Tukio hilo lilikuja baada ya David Moyes kumuonya Carballo kabla ya mchezo huo awe makini na mbinu za Bayern kujirusha.
Kocha wa United amesema: "Nafikiri Schweinsteiger alimchezea rafu Wayne. Ilikuwa ni kadi ya njano- au angalau faulo tu,".
Lakini United pia ilikuwa na bahati baada ya kunusurika kumpoteza mchezaji mmoja, kufuatia Antonio Valencia kuepuka kadi ya pili ya njano kwa kumchezea rafu Jerome Boateng. Moyes, pamoja na hayo, alimtetea mchezaji wake kwa kusema: "Kijana aliufuata mpira miguuni mwa Antonio Valencia,".
Mtu anajirusha, unatoa kadi: Pep Guardiola akibishana na refa baada ya kadi nyekundu
Nenda nje: Carlos Velasco Carballo akimuonyesha kadi nyekundu Schweinsteiger
Schweinsteiger alisawazisha bao la kuongoza la United lililofungwa na Nemanja Vidic na kuiweka Bayern katika nafasi nzuri ya kushinda nyumbani ili kusonga mbele.
Lakini Moyes alionyesha ana imani kubwa kwamba United inaweza kufika Nusu Fainali katika msimu ambao imeshuhudiwa wakisuasua katika Ligi Kuu ya England.
"Wakati wote nafikiri tutafunga bao dhidi yao na nitakwenda Munich nikiamini tutafunga goli,"alisema.
"Kuelekea kwenye mchezo huu, watu wengi waliipa nafasi Bayern kushinda kwa urahisi, wao ni mabingwa wa Ulaya. "Lakini usiku huu tumeonyesha tunaweza kufika huko, tutakwenda kula nao sahani moja ili kuhakikisha tunawatoa,".
"Tunahitaji kufunga. Tunahitaji kwenda huko kwa dhamira ya kushinda mechi. Timu nyingine zimekwishakwenda huko na kufanya hivyo, nasi tutahitaji kufanya hivyo hivyo,"alisema Moyes jana.
0 comments:
Post a Comment