Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi yupo Afrika Kusini kushiriki semina ya Shirikisho la Soka la kimataifa (FIFA) iliyoanza leo hadi Aprili 4 ambayo itahusu ushirikiano baina ya bodi hiyo ya soka duniani na Shirikisho la soka Afrika (CAF) katika maeneo kadhaa yakiwemo ya Ufundi.
Malinzi aliyeambatana na Katibu wake, Celestine Mwesigwa na Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi katika semina hiyo inayofaika Johannesburg, watakutana na Marais, Makatibu na Wakurugenzi wa Ufundi wa nchi nyingine pia wanachama wa CAF.
Zaidi ya Marais, Makatibu na Wakurugenzi wa Ufundi wa nchi 27 wanachama wa CAF zimealikwa kwenye semina hiyo, kipaumbele kikitolewa kwa nchi zinazozungumza Kiingereza.
Semina hiyo itafunguliwa na Katibu wa FIFA, Jerome Valcke na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA), Danny Jordaan.
Wakati huo huo: CAF itaendesha semina ya siku mbili kuanzia kesho kwa ajili ya Makamisaa wa mechi za wanaume kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016 mjini Cairo, Misri.
Semina hiyo itaelezea majukumu na haki za maofisa hao katika mechi, na kugusia maeneo mbalimbali kama utayarishaji wa mechi, kanuni za mashindano ya CAF, Masoko, Vyombo vya Habari na Marefa.
Pia mpango wa utawala wa elektroniki ujulikanao kama CAFCMS utazinduliwa na kuwasilishwa kwa washiriki, sambamba na mfumo wa leseni za klabu na wajumbe 110 kutoka vyama vya soka vya nchi 54 wanachama wa CAF watashiriki.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi |

0 comments:
Post a Comment