MSHAMBULIAJI Diego Costa anakabiliwa na mtihani wa kupambana na muda ili kuwa fiti kabla Atlético Madrid haijakutana na Chelsea katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuumia ugoko wakiifunga Getafe 2-0 jana.
Mshambuliaji huyo wa Hispania alitolewa nje baada ya kujigonga kwenye nguzo ya goli wakati akiifungia timu hiyo bao la pili katika La Liga.
Costa anaweza kukosa mechi dhidi ya The Blues zitakapokutana nchini Hispania Aprili 22, mwaka huu. Ushindi wa jana unaifanya Atletico ijisogeze jirani kabisa a ubingwa kwa kufikisha pointi 82 baada ya kucheza mechi 33, ikifuatiwa na Real Madrid yenye pointi 79 za mechi na Barcelona pointi 78 za mechi 33 pia.
Diego Costa alivyogonga nguzo wakati anafunga
Costa anapiga shuti ugoko unakwenda kugonga nguzo ya goli
Costa akiugulia maumivu
Costa anatolewa nje kwa machela
0 comments:
Post a Comment