// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); CANNAVARO NJE YANGA NA JKT OLJORO, MIKADI YA NJANO YAMPONZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE CANNAVARO NJE YANGA NA JKT OLJORO, MIKADI YA NJANO YAMPONZA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, April 10, 2014

    CANNAVARO NJE YANGA NA JKT OLJORO, MIKADI YA NJANO YAMPONZA

    Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
    YANGA SC itamkosa Nahodha wake wake, Nadir Haroub 'Cannavaro’ katika mchezo wa Jumapili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji JKT Oljoro mjini Arusha.
    Cannavaro alipewa kadi ya tatu ya njano katika mchezo wa jana dhidi ya Kagera Sugar na maana yake atarejea kwenye mechi ya kufunga msimu dhidi ya mahasimu, Simba SC.
    Tayari Yanga SC inamkosa beki wake mwingine wa kati, Kevin Yondan ambaye pamoja na wachezaji wengine, David Luhende, Haruna Niyonzima, Athumani Iddi ‘Chuji’ na Emmanuel Okwi hawapo kambini kwa sababu ambazo haswa hazieleweki.
    Kadi zimemponza; Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto hatakuwepo Yanga na Oljoro

    Yanga inatarajiwa kuondoka leo asubuhi kuelekea mjini Arusha kwa ajili ya kuifuata JKT Oljoro.
    Yanga na JKT Oljoro.
    Akizungumza na BIN ZUBEIRY leo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, amesema kwamba wanaenda Arusha kusaka ushindi tu.
    Pluijm alisema kuwa kamwe hawataidharau JKT Oljoro licha ya kuwa katika hatari ya kushuka daraja.
    “Tunaenda kupambana na si kitu kingine...tunahitaji kushinda mechi zote zilizosalia ili tujue hatma ya kutetea ubingwa wetu," alisema kocha huyo kutoka Uholanzi.
    Alieleza kwamba amewaandaa wachezaji wake kupata ushindi na kuwa makini kutumia nafasi zote watakazozitengeneza.
    Yanga sasa ina pointi 52 na baada ya mechi ya Jumapili itabakiza mchezo mmoja dhidi ya watani zao Simba itakayofanyika Aprili 19 mwaka huu na Azam FC ipo kileleni kwa pointi zake 53 ikiwa imebakiza mechi mbili, ukiwemo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CANNAVARO NJE YANGA NA JKT OLJORO, MIKADI YA NJANO YAMPONZA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top