// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BENADIR YATWAA UBINGWA WA SOMALIA BILA KUPOTEZA HATA MECHI MOJA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BENADIR YATWAA UBINGWA WA SOMALIA BILA KUPOTEZA HATA MECHI MOJA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, April 03, 2014

    BENADIR YATWAA UBINGWA WA SOMALIA BILA KUPOTEZA HATA MECHI MOJA

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    KLABU ya Banadir SC imetwaa ubingwa wa Somalia bila kupoteza hata mechi moja na ikiwa bado ina mcehzo mmoja mkononi.
    Taarifa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) iliyotumwa BIN ZUBEIRY, imesema kwamba timu hiyo ya Mogadishu imejihakikishia taji baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gaadiidka Jumatatu (Machi 30, 2014), baada ya kufikisha idadi ya pointi ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.
    Tutakutana Ligi ya Mabingwa; Benadir imetwaa mapema ubingwa wa Somalia 

    Timu zote zilicheza soka maridadi ya ushindani huku Gaadiidka ikipambana na kuepuka kushuka daraja.
    Baada ya kipindi cha kwanza kigumu, mshambuliaji mzaliwa wa Nigeria, Mustapha Maxwell Utangi aliifungia Banadair bao la kuongoza dakika ya 52 kabla ya Mkenya, Marcel Somson Otigi kufunga la pili dakika mbili baadaye.
    Banadir imemaliza ligi bila kufungwa hata mchezo mmoja kati ya mechi 13 ikikusanya pointi 31, sita zaidi ya Elman inayoshika nafasi ya pili na ina mchezo mmoja mkononi katika ligi hiyo inayoshirikisha timu nane. Savana ambayo imevuna pointi moja tu hadi sasa, imeshuka hadi daraja la pili ikielekea kwenye mechi ya mwisho Jumapili.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BENADIR YATWAA UBINGWA WA SOMALIA BILA KUPOTEZA HATA MECHI MOJA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top