// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BEKI AZAM AENDA AFRIKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BEKI AZAM AENDA AFRIKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 07, 2014

    BEKI AZAM AENDA AFRIKA KUSINI

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    BEKI wa pembeni wa Azam FC, Samih Hajji Nuhu ameondoka alfajiri ya leo kwenda Cape Town kupitia Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa goti la mguu wa kushoto.
    Tovuti ya Azam FC imeandika leo kwamba Nuhu ameongozana na Daktari Mkuu wa Azam FC, Dk Mwanandi Juma Mwankemwa pamoja na Mweka Hazina wa timu, Abdulkarim Shermohamed Bahadour maarufu kama Karim Mapesa.
    Safari njema; Haji Nuhu kulia akiwa na Dk Mwankemwa katikati na Karim Mapesa kushoto alfajiri ya leo JNIA

    Mzanzibari huyo atafanyiwa upasuaji katika hospitali ya Vincent Palocci mjini Cape Town na Mtaalamu, Dk. Nicholas, ambaye ameweza kuwarudisha uwanjani wachezaji wengi wa Afrika Kusini waliopata maumivu makubwa. 
    Hii itakuwa mara ya tatu kwa Nuhu kufanyiwa operesheni ya goti hilo, baada ya awali kufanyiwa mara mbili nchini India, kwanza katika hospitali ya Mumbai chini ya Dk. Tanna na ya pili hospitali ya Pune.
    Nuhu amekuwa nje ya Uwanja tangu mwaka jana na msimu huu wote hajagusa mpira kwa sababu ya maumivu hayo. Ni matarajio ya uongozi wa Azam kwamba tiba ya Afrika Kusini itamrejesha uwanjani mchezaji huyo kinda mwenye kipaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BEKI AZAM AENDA AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top