// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BARCELONA YAFUNGIWA KUSAJILI ULAYA, NI KWA KUSAJILI WATOTO KINYUME NA KANUNI ZA FIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BARCELONA YAFUNGIWA KUSAJILI ULAYA, NI KWA KUSAJILI WATOTO KINYUME NA KANUNI ZA FIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, April 03, 2014

    BARCELONA YAFUNGIWA KUSAJILI ULAYA, NI KWA KUSAJILI WATOTO KINYUME NA KANUNI ZA FIFA

    KLABU kubwa za Ligi Kuu Ulaya zimesema zimejisafisha baada ya Barcelona kufungiwa kufanya usajili wa wachezaji kwa kukiuka sheria za usajili kwa kusaini wachezaji walio chini ya umri wa miaka 18.
    Chelsea, Manchester United, Manchester City na Arsenal zimesema zote zitazingatia sheria za FIFA juu ya kusajili wachezaji wadogo katika soka ya England.
    Barcelona imezuiwa kusajili wachezaji katika vipindi viwili vijavyo vya usajili kwa kukiuka ibara ya 19 ya kanuni za FIFA za usajili.
    FIFA imeituhumu akademi ya Barcelona, iitwayo La Masia kwa kumsajili Mholanzi mwenye asili ya Nigeria aliye chini ya umri wa miaka 14, Bobby Adekanye; na Wakorea watatu walio chini ya umri wa miaka 15, Lee Seung Woo, Paik Seung-Ho na Jang Gyeolhee, Mfaransa Theo Chendri aliye chini ya umri wa miaka 16 na Mcameroon Patrice Sousia aliye chini ya umri wa miaka 14.
    Pigo: Wachezaji wa Barcelona, Lionel Messi na Cesc Fabregas ambao timu yao imefungiwa kusajili

    MAKINDA AMBAO HAWARUHUSIWI KUCHEZA BARCELONA

    Lee Seung Woo - Korea, Cadete B (U15s)
    Paik Seung-Ho -Korea, Cadete A (U16s)
    Jang Gyeolhee - Korea, Cadete B (U15s)
    Theo Chendri - Ufaransa, Cadete A (U16s)
    Patrice Sousia - Cameroon, Infantil A (U14s)
    Bobby Adekanye - Uholanzi Nigerian (U14s) 
    Barcelona pia imepigwa faini ya francs za Uswisi 450,000 na Chama cha Soka Hispania francs 500,000 kwa kuvunja kanuni za usajili wa mchezaji.
    Mabingwa hao wa Hispania walichunguzwa baada ya kusajili wachezaji 10 wadogo na kuwasajili kucheza mashindano kati ya mwaka 2009 na 2013.
    Uongozi wa Barcelona wamekuwa wakifuatiliwa tangu walipolazimishwa kusema usajili wa Neymar kutoka Santos ni Pauni Milioni 71.5million, na si Milioni 47.3, ukijumlisha na fedha alizolipwa Neymar na famili yake.
    Rais wa zamani wa Barca, Sandro Rosell, alilaumiwa kwa kuvunja kanuni za FIFA na katika sakata hilo, akalazimika kujiuzulu.
    Barcelona, washindi wa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa katika miaka 10 iliyopita, inamilikiwa na wanachama na inatambulika kama 'Ni zaidi ya klabu,’.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCELONA YAFUNGIWA KUSAJILI ULAYA, NI KWA KUSAJILI WATOTO KINYUME NA KANUNI ZA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top