MABAO mawili ya Lionel Messi katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Real Betis Uwanja wa Camp Nou usiku huu yameifanya Barcelona ipunguze pengo la pointi dhidi ya vinara wa La Liga, Atletico Madrid, hadi kubaki pointi moja.
Hata hivyo, Barca haikucheza soka ya kuvutia na ni Muargentia huyo pekee aliyekuwa bora uwanjani leo katika kikosi kizima cha Blaugrana wakikaza msuli kwenye mbio za ubingwa Hispania
Barcelona ikimalizia wiki ngumu baada ya kufungiwa kusajili na FIFA hadi mwaka 2015 walionekana kutotikiswa na adhabu hiyo kwa kuonyesha bango la kuunga mkono akademi yao, La Masia uwanjani kabla ya mechi.
Messi alifunga dakika za 15 na 85, wakati bao la tatu lilifungwa na Figueras aliyejifunga dakika ya 67, wakati bao la wapinzani lilifungwa na Ruben Castro dakika ya 68 na sasa Barca inatimiza pointi 78 baada ya kucheza mechi 32, wakati Atletico ipo kileleni kwa pointi moja zaidi za mechi 32 pia.
Real Madrid nayo imeendelea kupambana kufuatia ushindi wa mabao 4-0 ugenini dhidi ya Real Sociedad na kutimiza pointi 76 baada ya mechi 32. Mabao ya Real yamefungwa na Illarramendi dakika ya 45, Gareth Bale dakika ya 66, Pepe dakika ya 85 na Alvaro Morata dakika ya 88.

0 comments:
Post a Comment