// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); AZAM FC MABINGWA LIGI KUU LEO WAKIWAFUNGA RUVU NA YANGA WAKAFUNGWA KAGERA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE AZAM FC MABINGWA LIGI KUU LEO WAKIWAFUNGA RUVU NA YANGA WAKAFUNGWA KAGERA TAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, April 09, 2014

    AZAM FC MABINGWA LIGI KUU LEO WAKIWAFUNGA RUVU NA YANGA WAKAFUNGWA KAGERA TAIFA

    Na Mahmoud Zubeiry, Mlandizi
    AZAM FC inaweza kutawazwa kuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo, iwapo itaifunga Ruvu Shooting Uwanja wa Mabatini Mlandizi mkoani Pwani na wakati huo huo Yanga SC ikafungwa na Kagera Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Azam yenye pointi 53, ikishinda leo itafikisha 56 na mechi mbili mkononi ili kumaliza ligi, wakati Yanga iliyocheza idadi ya mechi sawa na Azam, ikisimamishwa leo na pointi zake 49 ilizonazo hata ikishinda mechi zake zilizosalia itafikisha 55.
    Mabingwa? Azam FC wanaweza kutawazwa mabingwa leo iwapo washinda Mlandizi na wapinzani wao Yanga wakafungwa na Kagera

    Kwa maana hiyo timu ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inaweza kuwa bingwa mpya wa Ligi Kuu ya Bara.
    Labda Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaweza kuchelewa kutangaza rasmi bingwa kwa sababu ya malalamiko ambayo Yanga wamewasilisha dhidi ya mchezaji Mohammed Neto wa Mgambo JKT.
    Yanga inadaia Neto ambaye alicheza dhidi yao katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), Jumapili iliyopita si raia wa Tanzania na hana Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC), na ingawa malalamiko hayo yamewasilishwa nje ya muda (time barred), lakini TFF imeyapokea na imesema itayawasilisha kwenye Kamati husika kwa ajili ya kupitiwa na baadaye kutolewa uamuzi.
    Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko yote kuhusu mchezo yanatakiwa kuwasilishwa ndani ya saa 24 baada ya mchezo kumalizika na Yanga waliwasilisha malalamiko hayo nje ya muda.
    Lakini wazi kulingana na kanuni za Ligi Kuu, Yanga haiwezi kunufaika na pointi za chee baada ya kushindwa kwa kipigo cha 2-1 uwanjani.
    Aya ya kwanza ya kanuni ya 61 ya Ligi Kuu ya Bara inayozungumzia adhabu zinazohusu usajili na uhamisho inasema; “Mchezaji yeyote atakayebadili jina lake halisi kwa madhumuni ya kudanganya ili asajiliwe kinyume cha masharti ya Kanuni hizi, atafungiwa kucheza mpira ndani na nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi kumi na miwili kuanzia tarehe ya kubainika,”. Aya ya pili ya kanuni hiyo inasema; “Klabu iliyomchezesha mchezaji aliyebadili jina kwa nia ya kudanganya italipa faini ya TShs 1,000,000/= kwa kila mchezo ambao mchezaji huyo alicheza, lakini matokeo ya uwanjani hayatobadilika,”.
    Kwa kanuni hizi- maana yake Yanga SC haitanufaika na pointi za chee baada ya kufungwa 2-1 na Mgambo JKT katika mchezo huo wa Ligi Kuu iwapo itabainika Neto alidanganya jina ili kusajiliwa na Mgambo kwa kukwepa ugumu wa kupata ITC.
    Lakini kanuni hiyo hiyo aya ya tatu inasema; “Klabu itayothibitika kumchezesha mchezaji ambaye hajasajiliwa na klabu hiyo, itapoteza michezo husika, kitalipa faini ya shilingi milioni moja (1,000,000/=) na mchezaji husika atafungiwa kwa kwa kipindi kisichopunguwa miezi kumi na miwili (12) bila ya kujali kukatwa au kutokatwa rufaa,”.
    Kwa mujibu wa malalamiko ya Yanga SC, Neto au Melondo habanwi na aya ya tatu ya kanuni ya 61, bali adhabu yake inaweza kupatikana kutoka aya ya kwanza na ya pili ya kanuni hiyo, iwapo itabainika ni kweli alifanya udanganyifu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC MABINGWA LIGI KUU LEO WAKIWAFUNGA RUVU NA YANGA WAKAFUNGWA KAGERA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top