KATIKA dakika ya 90 – kutoka kwa Manchester United kukionekana wazi – alijikuta akiwa na mpira mguuni kwake. Alikuwa amesimama upande wa kushoto, Wayne Rooney alikuwa akijiandaa kupiga mpira wa adhabu.
Sekunde chache baadaye baada ya Manchester United kutokuvuna kitu kutokana na mpira wa adhabu hiyo, Rooney alikuwa kwenye eneo lake la hatari, akijaribu kumzuia Arjen Robben ambaye juzi alikuwa moto wa kuotea mbali.
Alimzuia kwa ufasaha mkubwa sana na alitia hamasa. Hakuna ambaye ataumizwa zaidi na matokeo ya Jumatano usiku zaidi ya Rooney. Nahodha mteule wa United kwa msimu ujao, hakuna ambaye angekimbia sana uwanjani zaidi yake.
Machungu: Rooney akitoka uwanjani akiwa na mawazo baada ya kiwango kibovu dhidi ya Bavaria
Wakati kocha wa United, David Moyes akiwa hatambua mustakabali wake, ni muhimu sana sasa hivi kumvumbua upya Rooney yule wa kitambo, mchezaji kinda ambaye alizaliwa kushinda mechi za soka. ni rahisi sana, Moyes anatakiwa kumrudisha Rooney yule tishio.
Jumatano usiku pale Bavaria, Rooney alipata nafasi kadhaa za kuibeba United katika nusu zote za mechi. Na mara zote hizo hakuonyesha dalili zozote za kufunga bao, licha ya uchovu wote huo ni wazi jamaa huyu mwenye miaka 28 alilala macho akifikiria makosa yake.
Nafasi ya kwanza ilikuja katika dakika ya 20 wakati alipopewa bonge la pande akiwa katikati. Huku Shinji Kagawa akiwa hana mtu upande wake wa kushoto, mabeki wa Bayern walivutika kwenye mpira, Rooney alitakiwa kutoa pasi.
Nje: Rooney akipaisha mpira wakati wa kipindi cha kwanza
Au hata kama alitaka kupiga pasi angalau angepiga shuti ambalo lilikuwa na ujumbe wake. Mwisho wa yote jamaa hakufanya lolote kati ya hayo na badala yake aliung’ang’ania mpira na kupiga kashuti cha kitoto na kuanzisha usiku mgumu aliokuwa nao usiku wa juzi.
Baadaye sana, wakati ambao United ilikuwa imeduwazwa na bao la kusawazisha la Bayern – Rooney alipata nafasi nyingi ya kuifungia United bao la kuongeza.
Kama angefunga bao hilo angeweza kuibeba United hadi kwenye hatua ya nusu fainali, lakini safari hii aliugusa mpira kidogo kama siyo kupiga wakati goli likiwa yadi 15 kutoka alipokuwepo. Kusema kwamba alipiga shuti utakuwa ni uongo. Kilikuwa kijishuti na kutoka hapo ilikuwa wazi majanga yalikuwa yanakuja kwa United.
Ngumi ya shingo: Kocha wa United, David Moyes alishuhudia timu yake ikipoteza uongozi ndani ya sekunde 60 tu.
Kadata: Rooney akizinguana na Arjen Robben wa Bayern baada ya kushindwa kufanya lolote kwenye mechi
Rooney alikuwa akipambana hadi mwisho, ndiyo. Maumivu tayari yalishaanza kuchukua nafasi ya sindano za maumivu alizochomwa kutokana na kuvunjika kidole. Ukweli ni kwamba japokuwa Rooney alionekana kuchoka kama mchezaji Jumatano usiku.
Msimu mrefu – majeruhi ya mara kwa mara yameanza kumuathiri Rooney na kwa mara nyingine inaonekana kana kwamba staa huyo wa England anaenda kwenye Kombe la Dunia huku akiwa ameshachoka tayari.
Kwa kifupi hili ni tatizo kwa England. Kombe la Dunia kwao litakuwa majanga kama wataenda wakati mchezaji wao muhimu akiwa yuko kwenye kiwango kibovu.
Kwa United ukiangalia kwa jicho la mbali ni wazi kuwa Rooney ni tatizo ambalo linahitaji kutatuliwa.
Basi tena: Rooney na wachezaji wenzake wa United wakiwa wamekata tamaa baaad ya Bayern kufunga bao la tatu
Mchezaji muhimu: David Moyes na United inamuhitaji awe kwenye kiwango chake
Vita pale Bavaria: Rooney akiruka kupambana na Dante
Kuelekea mbele hili ni lazima libadilike. Kuna kila dalili kuwa Rooney atakuwa nahodha wa United msimu ujao na bila kujali mchezaji gani atasajiliwa na Moyes wakati wa kiangazi – Rooney ataendelea kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Old Trafford. Moyes atatengeneza timu yake kumzunguka na hilo litakuwa muhimu kama akipatia.
Kwa kipindi kirefu, United imenufaika kwa tabia ya Rooney kutokuwa mbinafsi na ari yake ya kukimbia uwanja mzima. Mshambuliaji wa kweli, hutumia nguvu zake katika eneo sahihi kwa wakati muafaka.
Huwa hawapati nafasi ya kushinda mechi kama Rooney aliyoipata usiku wa jana wakati zikiwa zimesaliwa dakika 15 halafu wakazipoteza kizembe.
Matukio yalikuwa yakipekee Jumatano usiku na hilo ni lazima lisemwe.
Jikaze: Moyes akimpa Rooney maelekezo
Ukikutana na timu ambayo kiufundi imekuzidi sana, Moyes alihitaji kutumia mbinu ambazo ni za kujipanga zaidi na za vitendo. Walihitaji kupaki basi.
Rooney ni lazima angetoa mchango wake katika hilo.
Kwa mfani katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, Rooney akiwa amesimama nje ya D, Rooney – ndiye alikuwa mchezaji wa mbele zaidi wa United, wakati Jerome Boateng – alikuwa amesimama yadi 10 katika nusu ya United kama beki wa mwisho wa Bayern.
Ilishangaza kuangalia kuna wakati, lakini ilijulikana kuwa itakuwa hivyo na ilielewejka. Huu haukuwa usiku wa kucheza soka la United ya zamani soka la kushambulia au kakabia juu.
Guardiola: It's hard to play against eight men in the box
Chini ya kiwango: Rooney aliharibiwa na majeruhi
Kuponda siyo vizuri kuwa kuna wakati, hasa inapotokea staa wa kikosi chako akazingua. Moyes hataweza kumlaunu Rooney na hilo ni sahihi, japokuwa amezungumzia nafasi ya pili aliyokosa Rooney ilivyokuwa muhimu.
Haijalishi kama Rooney alikuwa na matatizo ya Afya Jumatano usiku hilo linaweza kuzua mjadala baadaye, lakini alionekana kuwa mzima tu.
Siku hizi Rooney hajafikia kile kiwango ambaco watu walitarajia atakuwa nacho katika miaka hii na hilo ndilo tatizo la kutia hofu.
0 comments:
Post a Comment