// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ALLY BUSHIRI KOCHA BORA LIGI KUU ZANZIBAR, WADHAMINI WAMCHAFUWA NA ‘KAMILIONI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ALLY BUSHIRI KOCHA BORA LIGI KUU ZANZIBAR, WADHAMINI WAMCHAFUWA NA ‘KAMILIONI’ - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, April 09, 2014

    ALLY BUSHIRI KOCHA BORA LIGI KUU ZANZIBAR, WADHAMINI WAMCHAFUWA NA ‘KAMILIONI’

    Na Ameir Khalid, Zanzibar
    KOCHA Ali Bushiri wa timu ya KMKM iliyotwaa kwa ubingwa wa ligi kuu ya Zanzibar Grand Malt msimu wa 2013/2014, ametajwa kuwa kocha bora na kuzawadiwa kitita cha shilingi milioni moja na wadhamini wa ligi hiyo kinywaji cha Grand Malt.
    Bushiri ameiongoza KMKM kwa misimu mitatu ambapo alimudu kuipa ubingwa mwaka 2012/2013, na huu wa juzi ni wa pili mfululizo kwake.
    Kocha huyo aliyewahi kuwa msaidizi wa kocha mkuu wa timu ya taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’ Mabrazili Marcio Maximo, na kwa pamoja walimudu kuibadilisha timu hiyo licha ya kukosa mataji au kufuzu fainali za mataifa ya Afrika.

    Kocha Ali Bushiri wa KMKM, akipokea hundi ya shilingi milioni moja alizozawadiwa na wadhamini wa ligi kuu ya soka Zanzibar Grand Malt wakati wa tafrija ya kuwapongeza washindi na wote waliofanikisha ligi msimu wa 2013/2014 iliyofanyika Chuo cha Maendeleo ya Utalii Zanzibar, Maruhubi mwishoni mwa wiki. Anayekabidhi hundi hiyo ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar (BTMZ) Khamis Abdallah Said. (Picha na Ameir Khalid).

    Hata hivyo, wawili hao waliweza kuipeleka Taifa Stars katika mashindano ya bara hilo yanayoshirikisha wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) mwaka 2009 yaliyofanyika nchini Ivory Coast ingawa timu hiyo haikuvuka hatua ya makundi.
    Bushiri alitangazwa kuwa kocha bora wakati wa tafrija ya kutoa zawadi kwa washindi, iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Maendeleo ya Hoteli na Utalii Maruhubi usiku wa Jumapili iliyopita.
    Mlinda mlango huyo wa zamani wa klabu za Small Simba, Malindi, na timu za taifa Zanzibar na Tanzania, amekumbana na changamoto mbalimbali katika harakati zake, ikiwemo kufungiwa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa miaka mitano kuongoza timu katika mashindano ya kimataifa, adhabu ambayo iliongezwa nguvu na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA).
    Akionesha ujasiri, uvumilivu na kutokata tamaa,  Bushiri amekuwa kocha wa kupigiwa mfano kwani kutokana na malengo aliyonayo, ameweza kushinda vikwazo mbalimbali ndani na nje ya viwanja.
    Aidha katika tafrija hiyo, klabu ya KMKM iliyotwaa ubingwa wa ligi kuu ilikabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi, na makamu bingwa timu ya Polisi ilitunukiwa hundi ya  shilingi milioni tano.
    Mfaume Ali aliyeteuliwa kuwa mwamuzi bora wa mashindano ya mwaka huu, naye aliondoka na kitita cha shilingi milioni moja.
    Mchezaji Amour Omar ‘Janja’ wa Miembeni SC amekunja shilingi milioni moja baadaya kuibuka mfungaji bora kwa kupachika  mabao 14.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALLY BUSHIRI KOCHA BORA LIGI KUU ZANZIBAR, WADHAMINI WAMCHAFUWA NA ‘KAMILIONI’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top