MASHABIKI wa Arsenal hivi karibuni watamuona tena uwanjani kiungo Abou Diaby akiichezea timu yao, baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka kutokana na maumivu ya goti.
Maumivu ya mguu yalimuweka nje kwa muda huo mrefu mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa na sasa anapambana kwa mazoezi makali ya kujiweka fiti ili kuanza kazi tena.
Mashabiki hawana furaha na Diaby kwa sababu katika kipindi cha miaka minane ya kuwa na klabu hiyo, ametumia muda mwingi zaidi kuwa nje ya kikosi kutokana na majeruhi.
Lakini picha alizopigwa hivi karibuni mjini Paris, Ufaransa zinamuonyesha akifanya mazoezi makali ya kujiweka fiti baada ya kupona ili kurejea uwanjani.
Mbio: Kiungo huyo wa Arsenal akikimbia kujiweka fiti
Mazoezi makali: Diaby akifanya mazoezi ya misuli
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Paris hajachezea kikosi cha kwanza cha Arsenal tangu aumie goti katika mchezo dhidi ya Swansea Machi mwaka jana.
Lakini picha hizi zinaweza kumtuliza kocha Arsene Wenger na kuwajengea imani mashabiki wa timu hiyo ya Uwanja wa Emirates, baada ya kumuona Diaby akifanya mazoezi kamili ya nguvu kama kukimbia na kujenga misuli huku akiwa mwenye tabasamu.
Kazi kazi: Diaby akijifua vikali
Diaby yuko karibu kurejea uwanjani tangu aumie goti Machi mwaka jana
Wenger amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo asubuhi kwamba hatamuharakisha Diaby kurejea uwanjani baada ya kupona.
Kiungo huyo aliripotiwa kupata matatizo ya nyonga wakati akikichezea kikosi cha vijana cha Arsenal chini ya umri wa miaka 21 dhidi ya Chelsea katikati ya wiki ambayo itamfanya aukose mchezo wa Jumatatu dhidi ya Newcastle.
"Diaby alicheza kipinchi kimoja (kikosi cha U21),"alisema Wenger makao makuu ya timu hiyo, Colney mjini London. "Bado ana mudea gani kurejea ni vigumu kusema, lakini alipata matatizo kidogo ya nyonga baada ya mechi hiyo,hivyo hatakuwepo Jumatatu," alisema Wenger.
Diaby cuts akimtoka Ruben Loftus-Cheek wa Chelsea katika mechi ya U21 Jumanne wiki hii
Diaby amekuwa nje ya Uwanja kwa zaidi ya mwaka tangu aumie
0 comments:
Post a Comment