MAGWIJI wa soka, Zinedine Zidane na Ronaldo kwa mara nyingine waliungana katika All-star kucheza mechi ya kupiga vita umasikini.
Sasa ni mwaka wa 11, Zidane na Ronaldo waliungana na nyota kama Fernando Hierro, Paolo Maldini, Pavel Nedved na Luis Figo.
Walimenyana na Young Boys mjini Bern, kikosi cha Zidane kikaibuka na ushindi wa mabao 8-6, shukrani kwake mshindi huyo wa Kombe la Dunia na Ufaransa kwa kufunga mabao mawili.
Mtaalamu: Zidane alifunga mabao mawili katika ushindi wa 8-5 dhidi ya Young Boys Bern XI
Nahodha: Ronaldo akifanya vitu vyake
KIKOSI CHA KWANZA CHA ALL STARS YA SHIRIKA LA UMOJA WA MATAIFA MRADI WA MAENDELEO
Antonios Nikopolidis (Ugiriki)
Michel Salgado (Hispania), Fernando Hierro (Hispania), Fabio Cannavaro (Italia), Paolo Maldini (Italia),
Luis Figo (Ureno), Zinedine Zidane (Ufaransa), Gennaro Gattuso (Italia), Pavel Nedved (Jamhuri ya Czech)
Ronaldo (Brazil), Davor Suker (Croatia)
Mshambuliaji wa zamani wa Borussia Dortmund na Uswisi, Stephane Chapuisat aliyekuwa Nahodha wa timu ya Young Boys iliyowajumuisha Hakan na Murat Yakin, alifunga mabao matatu peke yake kipindi cha kwanza, akimtungua vizuri Antonios Nikopolidis.
Kocha wa timu ya Zidane, Rais wa UEFA, Michel Platini, aliwapa mawaidha mazuri wachezaji wake wakati wa mapumziko na kipindi cha pili wakarejea na moto hadi kushinda.
Mwanasoka Bora wa Dunia wa kike mara tano, Marta aliingia kipindi cha pili na kwenda kufanya kazi nzuri akiwatengenezea nafasi za kufunga Zidane na baadaye Christian Vieri.
Michel Platini alikuwa kocha wa timu ya akina Zidane na Ronaldo
Mawili: Kiungo wa zamani wa Bolton, Youri Djorkaeff alifunga mabao mawili
Mbio mtindo mmoja: Ronaldo akimtoka Alain Rochat
Mkali: Mwanasoka Bora wa kike mara tano wa FIFA, Marta alipika mabao mawili
Kisha Vieri akafunga bao lake la pili kabla ya mvua mabao kutkapande zote hadi magwiji wakaachwa kwa 5-3.
Baadaye wakazinduka na kiungo wa zamani wa Bolton, Youri Djorkaeff akafunga mawili moja baada ya gonga safi kati yake na Zidane zilizowaduwaza mabeki wa Young Boys.
Hakan Sukur, aliyechezea kwa muda Blackburn Rovers, pia alifunga kabla ya Zidane kufunga bao lake la pili usiku huo kwa penalti.
Nyota mwingine wa zamani wa Rovers, Nuno Gomes, pia alifunga mechi hiyo ikiisha kwa magwiji kushinda 8-5.
Wachezaji wengine wenye majina makubwa usiku wa jana ni pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Davor Suker, kiungo wa Milan, Gennaro Gattuso na winga wa Liverpool na Real Madrid, Steve McManaman.
0 comments:
Post a Comment