Na Waandishi Wetu, Dar es Salaam na Morogoro
YANGA SC imeshindwa kuifunga Mtibwa Sugar pungufu leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, wakati Azam FC imeshinda mabao 4-0 dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mtibwa Sugar ilipata pigo dakika ya 56 baada ya mshambuliaji wake, Abdallah Juma kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumpiga kisukusuku au kipepsi, beki wa Yanga SC Kevin Yondan.
Hata hivyo, Mtibwa Sugar inayofundishwa na kocha kijana, Mecky Mexime ilijipanga vizuri kudhibiti mashambulizi ya Yanga hadi mwisho wa mchezo. Hussein Javu aliyetokea benchi na Simon Msuva walikosa mabao ya wazi dakika za mwishoni, wakati Emmanuel Okwi pia alikosa bao la wazi dakika ya 90 baada ya kupiga kichwa mpira ukagonga mwamba na kurudi uwanjani.
Matokeo haya yanaifanya Yanga SC ijiongezee pointi moja na kutimiza 39 baada ya kucheza mechi 18, hivyo kurejea nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao, kwani Mbeya City pia ina pointi 39.
Aidha, Yanga imeendeleza rekodi yake ya kutoshinda Uwanja wa Jamhuri Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar kwa mwaka wa tano sasa.
Septemba 19 mwaka 2009 ndipo Yanga SC iliposhinda kwa mara ya mwisho Uwanja wa Jamhuri wakati huo ikiwa chini ya kocha Mserbia, Profesa Dusan Savo Kondic na tangu hapo kila inapokwenda huko matokeo mazuri kwao yamekuwa sare.
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, hadi mapumziko tayari Kipre Herman Tchetche alikuwa amekwishamtungua mara mbili kipa Said Lubawa wa Coastal Union.
Mshambuliaji huyo kutoka Ivory Coast ambaye sasa anatimiza mabao 13 katika Ligi Kuu msimu huu, alifunga bao la kwanza dakika ya 21 baada ya kupata pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na kumlamba chenga maridadi kiungo Mkenya Jerry Santo na baadaye kipa Lubawa.
Ndugu huyo wa mchezaji mwingine wa Azam, Kipre Michael Balou alifunga bao la pili akimalizia krosi maridadi ya beki wa kushoto, Gadiel Michael dakika ya 38.
Kipindi cha pili, Azam tena waliendelea kuwanyanyasa Coastal na kufanikiwa kunenepesha ushindi wao.
Pasi nzuri ya Kipre Tchetche ilimkuta katika nafasi nzuri John Raphael Bocco ‘Adebayor’ akamtungua Said Lubawa kuipatia Azam bao la tatu dakika ya 64.
Wakati refa anajiandaa kupuliza filimbi ya kumaliza mchezo, mshambuliaji aliyepandishwa kutoka kikosi cha pili, Kevin Friday aliifunga bao la nne Azam FC pasi ya Kipre Tchetche.
Azam sasa inajichimbia kileleni kwa kutimiza pointi 43 baada ya kucheza mechi 19.

Wauaji; Kipre Tchetche aliyefunga mabao mawili kulia akimpongeza John Bocco katikati aliyefunga bao la tatu. Kushoto ni Kipre Balou. |

0 comments:
Post a Comment