Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
YANGA SC imepoteza dola 70,000 za Kimarekani, zaidi ya Sh. Milioni 100 za Tanzania kutokana na kampuni ya MGB ya Misri kushindwa kurusha moja kwa moja mechi yao dhidi ya Al Ahly ya Misri Jumamosi.
Yanga SC iliingia Mkataba wa dola 90,000 na kampuni hiyo kwa ajili ya kuonyesha mechi hiyo ya kwanza ya kuwania kucheza hatua ya 16 Bora kwa nchi za Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati na ikapewa malipo ya awali dola 20,000.
Mwakilishi wa kampuni ya MGB, Francis Gaitho alikuwa wa kwanza kuwalalamikia Yanga SC jana kukwamisha zoezi la kurusha mechi hiyo, akidai waliwafukuza uwanjani kampuni ya Star TV na kamera zao waliokwenda kufanya zoezi hilo.
Gaitho alisema baada ya kusaini Mkataba na Yanga, waliwalipa fedha za awali kutoka kwenye akaunti yao nchini Misri kwenda kwenye akaunti ya klabu hiyo Tanzania.
Hata hivyo, akasema timu ya watu wa utayarishaji waliotakiwa kuja kurekodi mchezo huo ilishindwa kufika nchini kwa wakati kutoka Cairo, hivyo wakalazimika kutafuta kampuni ya hapa Tanzania kufanya kazi hiyo na Star TV ikabahatika kupata tenda hiyo.
Gaitho akasema kwamba licha ya barua ya Ubalozi wa Misri kwamba MGB italipa malipo yaliyobaki baada ya mechi na kudhaminiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Yanga SC waligoma mechi hiyo kurekodiwa.
“Wakati tulipofikia mwafaka na kukubaliana mechi irekodiwe, bahati mbaya Star TV walikuwa tayari wamekwishaondoka uwanjani na muda ulikuwa umeenda,”alisema Gaitho.
Akalaani kwamba kukwama kuonyeshwa kwa mechi hiyo hakujawaathiri Watanzania pekee, bali na Wamisri pia katika wakati huu ambao nchi zinajaribu kujenga uhusiano mzuri baina yao, na hususan kwenye soka zama hizi ambazo wachezaji wananunuliwa.
“Ilikuwa ni fursa nzuri kwa wachezaji wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na pengine wangeweza kuzivutia klabu za nje zikawasilisha ofa ya kuwanunua katika klabu yao na kusaidia kukuza pato la klabu yao,”alisema.
Akijibu madai hayo ya Gaitho, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Mussa Katabaro alisema kwamba makubaliano yao na kampuni hiyo baada ya malipo ya awali ya dola 20,000 ilikuwa ni kulipa dola 35,000 kabla ya mechi na dola 35,000 nyingine baada ya mechi, lakini wakashindwa kutekeleza kipengele hicho cha Mkataba.
“Na mbaya zaidi, katika Mkataba wetu na wao tulikubaliana hakuna kupelekana Mahakamani, sasa tulipoona wameshindwa kulipa zile fedha, tukawazuia hadi walipe,”alisema Katabaro.
Kiongozi huyo wa Yanga amesema wateja wao pia hawakuwa wakweli katika maelezo yao walisema kuna mtu alikuwa anakuja na fedha kutoka Misri akakamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo, lakini walipofuatilia wakagundua si kweli.
Katabaro akasema baadaye wakadai Ubalozi wa Misri utalipa hizo fedha, lakini walipouliza wakakana na ndipo baadaye, TFF ikajitolea kuwaandikia Yanga SC hundi ya dola 35,000 na dola 10,000 kwa Stars TV ili mechi ionyeshwe.
“Sisi tulikubali kupokea hundi ya TFF mechi ionyeshwe, lakini Star TV wakagoma kupokea hundi ya TFF wakaondoka, sisi hatukuwafukuza kama wanavyodai hao jamaa. Kimsingi ni kwamba, hawa jamaa wametukosesha fedha dola 70,000. Kwa sababu pia baada ya kuwapa wao Mkataba, kuna kampuni nyingine ya Misri ikajitokeza ikiwa tayari kutupatia dola 100,000 kununua haki za TV za hiyo mechi, lakini sisi tukaheshimu Mkataba wetu na MGB, ila mwisho wa siku uungwana wetu umetuponza,”alisema Katabaro.
Katabaro alisema yaliyotokea katika sakata hilo yamewaachia fundisho kubwa na hawatarajii kurudia makosa.
Yanga SC iliyoshinda 1-0 katika mechi hiyo, inaingia kambini leo hoteli ya Bahari Beach, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kuanza maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaofanyika mwishoni mwa wiki mjini Cairo.
Tayari baadhi ya Maofisa wa Yanga SC wamekwishatangulia Cairo kwenda kuandaa mazingira ya timu itakapokuwa huko, ili kuepuka kufanyiwa hujuma na wenyeji.
YANGA SC imepoteza dola 70,000 za Kimarekani, zaidi ya Sh. Milioni 100 za Tanzania kutokana na kampuni ya MGB ya Misri kushindwa kurusha moja kwa moja mechi yao dhidi ya Al Ahly ya Misri Jumamosi.
Yanga SC iliingia Mkataba wa dola 90,000 na kampuni hiyo kwa ajili ya kuonyesha mechi hiyo ya kwanza ya kuwania kucheza hatua ya 16 Bora kwa nchi za Kaskazini mwa Afrika na Mashariki ya Kati na ikapewa malipo ya awali dola 20,000.
Mshambuliaji wa Yanga SC, Emmanuel Okwi kulia akimtoka beki wa Al Ahly Jumamosi |
Gaitho alisema baada ya kusaini Mkataba na Yanga, waliwalipa fedha za awali kutoka kwenye akaunti yao nchini Misri kwenda kwenye akaunti ya klabu hiyo Tanzania.
Hata hivyo, akasema timu ya watu wa utayarishaji waliotakiwa kuja kurekodi mchezo huo ilishindwa kufika nchini kwa wakati kutoka Cairo, hivyo wakalazimika kutafuta kampuni ya hapa Tanzania kufanya kazi hiyo na Star TV ikabahatika kupata tenda hiyo.
Gaitho akasema kwamba licha ya barua ya Ubalozi wa Misri kwamba MGB italipa malipo yaliyobaki baada ya mechi na kudhaminiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Yanga SC waligoma mechi hiyo kurekodiwa.
“Wakati tulipofikia mwafaka na kukubaliana mechi irekodiwe, bahati mbaya Star TV walikuwa tayari wamekwishaondoka uwanjani na muda ulikuwa umeenda,”alisema Gaitho.
Akalaani kwamba kukwama kuonyeshwa kwa mechi hiyo hakujawaathiri Watanzania pekee, bali na Wamisri pia katika wakati huu ambao nchi zinajaribu kujenga uhusiano mzuri baina yao, na hususan kwenye soka zama hizi ambazo wachezaji wananunuliwa.
“Ilikuwa ni fursa nzuri kwa wachezaji wa Tanzania kuonyesha vipaji vyao Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na pengine wangeweza kuzivutia klabu za nje zikawasilisha ofa ya kuwanunua katika klabu yao na kusaidia kukuza pato la klabu yao,”alisema.
Akijibu madai hayo ya Gaitho, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga SC, Mussa Katabaro alisema kwamba makubaliano yao na kampuni hiyo baada ya malipo ya awali ya dola 20,000 ilikuwa ni kulipa dola 35,000 kabla ya mechi na dola 35,000 nyingine baada ya mechi, lakini wakashindwa kutekeleza kipengele hicho cha Mkataba.
“Na mbaya zaidi, katika Mkataba wetu na wao tulikubaliana hakuna kupelekana Mahakamani, sasa tulipoona wameshindwa kulipa zile fedha, tukawazuia hadi walipe,”alisema Katabaro.
Kiongozi huyo wa Yanga amesema wateja wao pia hawakuwa wakweli katika maelezo yao walisema kuna mtu alikuwa anakuja na fedha kutoka Misri akakamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo, lakini walipofuatilia wakagundua si kweli.
Katabaro akasema baadaye wakadai Ubalozi wa Misri utalipa hizo fedha, lakini walipouliza wakakana na ndipo baadaye, TFF ikajitolea kuwaandikia Yanga SC hundi ya dola 35,000 na dola 10,000 kwa Stars TV ili mechi ionyeshwe.
“Sisi tulikubali kupokea hundi ya TFF mechi ionyeshwe, lakini Star TV wakagoma kupokea hundi ya TFF wakaondoka, sisi hatukuwafukuza kama wanavyodai hao jamaa. Kimsingi ni kwamba, hawa jamaa wametukosesha fedha dola 70,000. Kwa sababu pia baada ya kuwapa wao Mkataba, kuna kampuni nyingine ya Misri ikajitokeza ikiwa tayari kutupatia dola 100,000 kununua haki za TV za hiyo mechi, lakini sisi tukaheshimu Mkataba wetu na MGB, ila mwisho wa siku uungwana wetu umetuponza,”alisema Katabaro.
Katabaro alisema yaliyotokea katika sakata hilo yamewaachia fundisho kubwa na hawatarajii kurudia makosa.
Yanga SC iliyoshinda 1-0 katika mechi hiyo, inaingia kambini leo hoteli ya Bahari Beach, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kuanza maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaofanyika mwishoni mwa wiki mjini Cairo.
Tayari baadhi ya Maofisa wa Yanga SC wamekwishatangulia Cairo kwenda kuandaa mazingira ya timu itakapokuwa huko, ili kuepuka kufanyiwa hujuma na wenyeji.
0 comments:
Post a Comment