Na Salum Vuai, Zanzibar
KIKOSI cha Yanga SC kimeondoka asubuhi leo Cairo kuelekea mjini Alexandria, Misri tayari kwa mchezo wa marudiano, Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Al Ahly.
Kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans van der Pluijm ni mwenye kujiamini kuelekea mchezo huo akiwa na kipaumbele cha ushindi wa 1-0 katika mchezo wa nyumbani wiki iliyopita Dar es Salaam.
Yanga SC ilifikia katika hoteli ya Nile Paradise Inn waliyokodi wenyewe kwa msaada wa Balozi wa Tanzania nchini Misri, Mohammed Hamza na kuachana na hoteli waliyoandaliwa na wenyeji wao, Baron.
Mchezo huo, unatarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Border Guard (Haras El Hodood) unaomilikiwa na jeshi la nchi hiyo kuanzia Saa 1:00 usiku kwa saa za Misri kesho na Ahly tayari mjini Alexandria tangu jana.
Yanga SC leo wanatarajiwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Border Guard kwa mujibu wa kanuni, timu mgeni inaruhusiwa kuujaribu Uwanja wa mechi siku moja kabla ya mchezo.
Katika siku zake mbili za kuwa Cairo, Yanga SC ilikuwa ikifanya mazoezi yake kwenye Uwanja uliopo pembezoni mwa hoteli ya Nile usiku kwa kuwa mechi yenyewe itachezwa usiku.
Vurugu za mashabiki wa Al Ahly siku za karibuni zimefanya Mamlaka ya Jiji la Cairo kuwafungia ‘Mashetani Wekundu’ hao kucheza katika mji huo mkuu wa Misri.
Mashabiki wa Al Ahly walijeruhi Polisi 25 mwezi uliopita katika mchezo wa kuunganisha mataji ya klabu Afrika, maarufu kama CAF Super Cup wakiifunga CS Sfaxien ya Tunisia mabao 3-2 Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
Kwa ujumla mechi zote za soka Misri tangu mwaka 2013 alipong’olewa Rais Mohammad Mursi zimekuwa zikichezwa bila mashabiki na kesho pia itakuwa hivyo Yanga na Al Ahly.

0 comments:
Post a Comment