Na Salum Vuai, Zanzibar
YANGA SC ilitua mjini Alexandria majira ya Saa saba na ushei mchana na kupanga katika hoteli ya Sheraton tayari kwa mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Al Ahly utakaochezwa kwenye Uwanja wa Border Guard (Haras Hodoud ) kesho.
Yanga SC inayofundishwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm ilifikia Cairo Alhamisi na kuweka kambi katika hoteli ya Nile Paradise Inn ambako ilifanya mazoezi kwa siku mbili kabla ya leo kwenda Alexandria.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga SC, Clement Sanga alitangulia mjini Alexandria tangu jana asubuhi pamoja na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Misri kuandaa utaratibu wa timu hiyo kuishi mjini humo.
Tayari jioni hii kikosi cha Yanga SC kipo Uwanja wa Border Guard kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kuuzoea kwa mujibu wa kanuni, timu mgeni anaruhusiwa kufanya mazoezi katika Uwanja wa mechi siku moja kabla.
Taarifa kutoka kambi ya Yanga SC mjini Alexandria zinasema kwamba morali ya wachezaji iko juu kuelekea mchezo huo wa kukata na shoka na hakuna majeruhi hata mmoja.
Yanga SC inahitaji sare yoyote au kufungwa kwa tofauti ya mabao moja nayo ikifunga, mfano 2-1, 3-2, 4-3 ili kutinga Hatua ya 16 Bora, baada ya wiki iliyopita kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam, bao pekee la Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.

Wanaume wako tayari; Kikosi cha Yanga SC kilichoifunga 1-0 Al Ahly Dar es Salaam |

0 comments:
Post a Comment