Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inaendelea kesho (Machi 15 mwaka huu) kwa mechi tatu ambapo mabingwa watetezi Yanga wataumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Yanga SC watamkosa mshambuliaji wao tegemeo, Mrisho Ngassa ambaye aliumia katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Al Ahly mjini Alexandria. Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3 baada ya sare ya jumla ya 1-1, kila timu ikishinda 1-0 nyumbani kwake.
Nao vinara wa ligi hiyo, Azam wanaikaribisha Coastal Union ya Tanga katika mechi itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar es Salaam.
Mechi nyingine itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuwakutanisha wenyeji Kagera Sugar dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya.

Hatakuwepo; Mrisho Ngassa ataikosa mechi ya kesho kwa sababu ni majeruhi |
Mechi nyingine itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuwakutanisha wenyeji Kagera Sugar dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons kutoka jijini Mbeya.
0 comments:
Post a Comment