// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA NA AL AHLY HUENDA IKACHEZWA ALEXANDRIA, LAKINI WENYEJI HADI SASA HAWAJATHIBITISHA NA UGENI UPO CAIRO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA NA AL AHLY HUENDA IKACHEZWA ALEXANDRIA, LAKINI WENYEJI HADI SASA HAWAJATHIBITISHA NA UGENI UPO CAIRO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 06, 2014

    YANGA NA AL AHLY HUENDA IKACHEZWA ALEXANDRIA, LAKINI WENYEJI HADI SASA HAWAJATHIBITISHA NA UGENI UPO CAIRO

    Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
    YANGA SC wamefika salama leo Cairo tayari kwa mchezo wa marudiano Hatua ya timu 32 dhidi ya wenyeji, Al Ahly, Jumapili hii lakini mechi hiyo haitachezwa mjini humo kutokana na Mamlaka ya Jiji la Cairo kuwafungia mabingwa hao wa Afrika kucheza mechi zao huko kutokana na vurugu za mashabiki wake.
    Shirika la Habari la Ufaransa (AFP) limeandika leo kwamba, vigogo wa Misri, Al Ahly hawajui watacheza wapi mechi yao dhidi ya Yanga, zikiwa zimesalia siku tatu kabla ya mchezo wa kuwania Hatua ya 16 Bora.
    Tatizo hawa; Mashabiki wenye vurugu wa Al Ahly wamefanya mchezo wa marudiano baina ya timu yao hiyo na Yanga SC hadi sasa isieleweke utachezwa wapi

    Vurugu za mashabiki wake siku za karibuni zimefanya Mamlaka ya Jiji la Cairo kuwafungia ‘Mashetani Wekundu’ hao kucheza katika mji huo mkuu wa Misri.
    Mabingwa hao mara nyingi zaidi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, mara nane, Al Ahly wamechukua hatua kwa kujaribu kuuhamishia mchezo huo katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Alexandria kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano wa Raundi ya kwanza. 
    Lakini wakati muda ukikimbia kuelekea siku ya mchezo Jumapili, washindi hao wa mataji 18 tofauti ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) bado hawajathibitisha Uwanja wa kuufanyia mchezo huo.
    Mashabiki wa Al Ahly walijeruhi Polisi 25 mwezi uliopita katika mchezo wa kuunganisha mataji ya klabu Afrika, maarufu kama CAF Super Cup wakiifunga CS Sfaxien ya Tunisia mabao 3-2 Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.
    Kwa ujumla mechi zote za soka Misri tangu mwaka 2013 alipong’olewa Rais Mohammad Mursi zimekuwa zikichezwa bila mashabiki na hali hiyo pia inatarajiwa mwishoni mwa wiki hii — huku Al Ahly wakitafuta Uwanja wa muda kujaribu kukipiku kipigo cha 1-0 walichokipata kutoka kwa Yanga SC katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam Jumamosi.
    “Mamlaka haiko tayari kupokea mchezo wowote wa soka kwa sababu ya mashabiki baada ya kile kilichotokea kwenye mechi za karibuni za Ahly,” amekariwa na AFP Msemaji wa Chama cha Soka Misri (EFA), Azmi Megahed akisema.
    Ahly inayojaribu kutwaa taji la tatu mfululizo la Ligi ya Mabingwa msimu huu, ililazimishwa kucheza kwa kujihami zaidi katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
    Hata hivyo, wababe hao wa Misri walishindwa kumzuia Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kuiunganishia nyavuni kwa kichwa kona ya winga Simon Msuva akimtungua kipa hodari, Sherif Ekramy zikiwa zimesalia dakika saba mchezo kumalizika.
    Mshambuliaji chipukizi, Amr Gamal anaamini Ahly hawakuwa na bahati Jumamosi Dar es Salaam na anabashiri timu yake itazinduka katika mchezo wa marudiano na kuitoa Yanga SC.
    “Ulikuwa mchezo mgumu Tanzania, lakini hatukustahili kufungwa,” amekaririwa na AFP akisema. “Tutashinda nyumbani na kusonga Raundi ya Pili.”
    Zamalek, majirani wa Ahly mjini Cairo na mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa, pia hawako katika nafasi nzuri baada ya ushindi mwembamba nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya Kabuscorp ya Angola.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA AL AHLY HUENDA IKACHEZWA ALEXANDRIA, LAKINI WENYEJI HADI SASA HAWAJATHIBITISHA NA UGENI UPO CAIRO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top