KLABU ya Arsenal itamkabidhi tuzo ya kufanya muda mrefu zaidi kocha wao, Arsene Wenger akielekea kutimiza mechi ya 1,000 tangu aanze kupiga mzigo The Gunners.
Wenger, ambaye alianza kazi karika klabu hiyo Agosti mwaka 1996, atatimiza mechi hizo Jumamosi Uwanja wa Stamford Bridge na klabu hiyo itamkabidhi tuzo hiyo katika viwanja vya mazoezi, Colney mjini London kesho.
Taarifa kamili kuhusu kukabidhi tuzo hiyo zinafanywa siri, lakini tuzo hiyo itakabidhiwa wakati wa mazoezi kwa kuwa Mfaransa huyo hajataka hilo lichanganywe katika siku ya mechi.
Tuzo: Arsenal itampatia Arsene Wenger tuzo ya kufanya kazi muda mrefu akielekea kutimiza mechi ya 1,000 Jumamosi
Siku ya kwanza: Mfaransa huyo alichukua mikoba ya kuinoa Arsenal Agosti mwaka 1996
Mwenyekiti wa Arsenal, Sir Chips Keswick na Mwenyekiti wa Chama cha Makocha wa Ligi Kuu, Richard Bevan wote watahudhuria.
Katika miaka yake 18 ya kufanya kazi klabu hiyo ya London,Wenger ameshinda mechi 572, ametoa sare mechi 235 na kufungwa mechi 192 katika mechi 999 hadi sasa.
Pamoja na hayo, Wenger hajawahi kuifunga Chelsea ikiwa na kocha Mreno, Jose Mourinho, hadi sasa akiwa amefungwa mechi tano, sare tano katika mechi 10 baina yao.
Mourinho hajawahi kufungwa mechi nyumbani katika Ligi Kuu ya England akiwa kocha wa Chelsea, katika mechi 75 hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment