Na Prince Akbar, Dar es Salaam
MUOSHA huoshwa, naam. Usemi huo umetimia leo baada ya timu ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji iliyoitoa Azam FC ya Tanzania katika Raundi ya Awali ya Kombe la Shirikisho Afrika, nayo kutolewa katika Raundi ya Kwanza.
Ferroviario iliitoa Azam FC kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 2-0 Beira baada ya kufungwa 1-0 Dar es Salaam, lakini nayo safari yake imekomea leo baada ya kutolewa kwa jumla ya bao 1-0 na Zesco United ya Zambia.
Wiki iliyopita Ferroviario ililazimishwa sare ya bila kufungana na Zesco mjini Beira na leo imefungwa 1-0 mjini Lusaka, hivyo kuaga mashindano.
Katika mechi nyingine za leo, How Mine ya Zimbabwe imesonga mbele baada ya kuitoa St Michel United ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 5-1, ikishinda 3-1 leo ugenini baada ya kushinda 2-0 nyumbani wiki iliyopita.
Bayelsa United ya Nigeria imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-0 dhidi ya Kondzo ya Kongo iliyoupata leo nyumbani baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita.
ASEC Mimosa ya Ivory Coast imesonga mbele pia kwa ushindi wa jumla wa 3-1 baada ya sare ya 1-1 leo Abidjan dhidi ya CO Bamako ya Mali ikitoka kushinda 2-0 wiki iliyopita mjini Bamako.
Mechi kati ya Maghreb Fes ya Morocco na Medeama ya Ghana inaendelea Morocco usiku huu. Katika mechi ya kwanza Madeama ilishinda 3-0 nyumbani.
Na kesho, Ismailia ya Misri itaikaribisha MK Etancheite ya DRC baada ya sare ya bila kufungana kwenye mchezo wa kwanza ugenini wiki iliyopita. Petro Atletico ya Angola itaikaribisha Ebusua Dwarfs ya Ghana baada ya kufungwa 2-0 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita.
Wadi Degla ya Misri itakuwa mwenyeji wa AS Douanes ya Togo baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza, Djoliba FC ya Mali itakuwa mwenyeji wa Don Bosco ya DRC baada ya kufungwa 2-1 katika mchezo wa kwanza.
Warri Wolves ya Nigeria itakuwa mwenyeji wa Union Douala ya Cameroon baada ya kushinda 3-2 katika mchezo wa kwanza na CA Bizertin ya Tunisia itakuwa mwenyeji wa Desportivo Huila ya Angola baada ya ushindi wa 1-0 ugenini.
Katika mechi za jana, Etoile Sahel ya Tunisia imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya CARA ya Kongo ikishinda 3-0 leo Tunis baada ya kufungwa 1-0 katika mchezo wa kwanza na Al-Ahly Shendy ya Sudan imeaga baada ya kufungwa kwa penalti 5-4 na AS Kigali kufuatia kila timu kushinda 1-0 nyumbani kwake.

Muosha huoshwa; Ferroviario wametolewa Kombe la Shirikisho leo |

0 comments:
Post a Comment