Na Mwandishi Wetu, Lubumbashi
KLABU ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ina matumaini makubwa ya kusonga mbele, Hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakapomenyana na Astres de Douala ya Cameroon katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Kwanza kesho mjini hapa.
Mazembe ilifanikiwa kupata sare ya kufungana bao 1-1 ugenini na timu hiyo ya Magharibi mwa Afrika katika mchezo wa kwanza mwishoni mwa wiki iliyopita, tena wageni hao wakitangulia kupata bao kupitia kwa Mzambia Jonas Sakuwaha kabla ya Astres kusawazisha kupitia kwa Namatchoua Bidias.
Hiyo inamaanisha timu hiyo ya DRC inahitaji tu kutoruhusu nyavu zake kuguswa katika mchezo wa marudiano kesho Lubumbashi – ambako wana rekodi nzuri.
Wacameroon walitawala sehemu kubwa ya mchezo nyumbani, lakini wakashindwa kutumia nafasi nyingi walizotengeneza. Ikiwa watafanikiwa kupata bao la mapema la kuongoza kesho, watafufua matumaini ya kusonga mbele, lakini ni timu chache zimeweza kupata bao kwenye Uwanja wa Mazembe miaka ya karibuni.
Washambuliaji wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wote wako fiti kuisaidia Mazembe kusonga mbele kesho. Mazembe iliwazuia wawili hao kurejea Tanzania kuichezea timu yao ya taifa, Taifa Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Namibia mjini Windhoek Jumatano timu hizo zikitoka 1-1 ili wapate muda wa kujiandaa na wenzao kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Refa wa Uganda, Denis Batte atachezesha mechi hiyo. Mshindi wa jumla atasonga mbele ambako atakutana na ama Barrack Young Controller ya Liberia, au Sewe Sport ya Ivory Coast ambazo zilitoka sare ya 3-3 katika mchezo wa kwanza Liberia.

Mtambo wa mabao; Mbwana Ally Samatta yuko tayari kuisaidia TP Mazembe kusonga mbele kesho |

0 comments:
Post a Comment