// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 27, 2014

    TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGA

    Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.
    Rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, shughuli inayoendelea kwa sasa ni kupima udongo (soil test) na kuandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo (Sports Complex) ukiwemo uwanja wa mpira wa miguu na majukwaa yake.
    Rais wa TFF, Jamal Malinzi katikati

    Amesema TFF imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la kujenga kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa yake.
    “Pia Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara waliovamia uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial ground) mjini Moshi,”amesema Malinzi.
    Amesema TFF inawakumbusha viongozi wa vyama vya mikoa ambao hawajaomba maeneo ya kujenga vituo vya michezo vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu, waongeze jitihada za kufanya hivyo na shirikisho hilo litawaunga mkono.
    “TFF inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama tayari vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na kuendeleza maeneo kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu. TFF inaahidi kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu haitasita kufanya hivyo,”amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TFF YAANZA KUENDELEZA UWANJA WA TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top