// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TASWA YAUNDA KAMATI MPYA YA TUZO, BIN ZUBEIRY NDANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TASWA YAUNDA KAMATI MPYA YA TUZO, BIN ZUBEIRY NDANI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 19, 2014

    TASWA YAUNDA KAMATI MPYA YA TUZO, BIN ZUBEIRY NDANI

    Na Dina Ismail, Dar es Salaam
    KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) iliyokutana jijini Dar es Salaam wiki iliyopita ilikubaliana kufanya mabadiliko makubwa katika Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa kila mwaka na TASWA.
    Makamu Mwenyekiti TASWA, Egbert Mkoko ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, kikao kilijiridhisha kuwa tuzo za TASWA zina heshima kubwa na wanamichezo hapa nchini wanazithamini na kuzitegemea kuliko tuzo za aina nyingine zozote.
    Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY Blog, Mahmoud Zubeiry kulia akiwa na mshambuliaji wa TP Mazembe ya DRC, Mbwana Samatta kushoto

    Mkoko amesema, kikao kilikubaliana kuwa pamoja na hayo bado kuna changamoto mbalimbali kuhusiana na tuzo hizo, hivyo kuna haja ya kuhakikisha zinaboreshwa zaidi ya ilivyo sasa.
    Amesema kutokana na hali hiyo, kikao kiliunda Kamati Maalum ya watu 12 Kusimamia Tuzo hizo, ambayo itakuwa chini ya uenyekiti wa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TASWA, Rehure Nyaulawa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Redio 100.5 Times FM na ina wajumbe wengine 10 ambao si viongozi wa TASWA, lakini ni waandishi wazoefu wa habari za michezo, hivyo tunaamini wataleta ufanisi.
    Amesema jukumu la kamati hiyo pamoja na kuandaa mchakato wa upatikanaji wa Wanamichezo Bora wa Tanzania mwaka 2013 na kupanga tarehe ya kufanyika tuzo hiyo mwaka huu, lakini pia imepewa mamlaka ya kutazama mfumo wa tuzo ulivyo na ikiwezekana kuubadili kwa namna itakavyoona inafaa kwa maslahi ya chama na maendeleo ya michezo kwa ujumla.
    “Ni nia ya Kamati ya Utendaji ya TASWA kuona tuzo inakuwa bora na ambayo wadau wa michezo wataendelea kuiheshimu kwa kila hatua. Hivyo kuamua kuipa kamati hiyo mamlaka ya kuamua mambo ya msingi katika kuiboresha kwa mipango ya muda mfupi na mrefu,”amesema.
    Licha ya Mwenyekiti Nyaulawa, Mkoko amewataja wengine walioteuliwa kuunda kamati hiyo na vyombo vyao katika mabano ni Elizabeth Mayemba (Mwandishi wa Majira), Amour Hassan (Mhariri wa habari za Michezo-Nipashe), Dominick Isiji (Mhariri wa michezo-The African) na Rais wa Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU), ambaye pia ni mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Daily News, Mbonile Burton.
    Wengine ni Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY blog, Mahmoud Zubeiry, Athanas Kazige (Mwandishi Uhuru), Suleiman Jongo (Mwandishi-Citizens), Angela Msangi (Mwandishi TBC1) na Cosmas Mlekani (Mwandishi-Spotileo) na Tulo Chambo ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Riadha Tanzania (RT) na pia Mhariri wa habari za michezo wa gazeti la Tanzania Daima.
    Katibu wa kamati hiyo atakuwa Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando na kikao cha kwanza cha kamati kitafanyika jijini Dar es Salaam Jumatatu Machi 24, ambapo kitafunguliwa na Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto, ambaye kwa sasa yupo safarini.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TASWA YAUNDA KAMATI MPYA YA TUZO, BIN ZUBEIRY NDANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top