HAIJALISHI rangi ya jezi — Barcelona, Inter Milan au Chelsea —Samuel Eto’o ameendelea kufanya vitu.
Amekuwa na mafanikio makubwa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, akitwaa mataji matatu na msimu huu akijaribu kutwaa la nne.
Zama za kutawala kwa ufungaji wa mabao zimehama kwake na sasa ni zamu ya akina Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Zlatan Ibrahimovic na Robert Lewandowski.
Mimi tena: Eto'o aling'ara pia kwenye Ligi ya Mabingwa akiwa na Inter Milan
Bado yumo: Samuel Eto'o ameifungia bao la kwanza Chelsea jana katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Galatasaray
Hao ndio wakali wa mabao kwa sasa wakiwa na jezi za Real Madrid, Barcelona, Paris Saint-Germain na Borussia Dortmund wanafunga kila wiki.
Eto’o ni mzoefu na ni bao lake la dakika ya nne jana ambalo liliitengenezea mazingira ya ushindi Chelsea. Amekuwa mfungaji wao tegemeo.
Akiwa na umri wa miaka 32, au 37 kama alivyosema kocha wa Chelsea, Jose Mourinho anabaki kuwa mfungaji babu kubwa.
Eto’o amefanikiwa kufunga dhidi ya vigogo wa soka msimu huu akitikisa nyavu mara mbili dhidi ya Schalke kwenye mechi ya Kundi lao Ligi ya Mabingwa, alifunga la bao la ushindi dhidi ya Liverpool na baadaye hat-trick dhidi ya Manchester United.
Katika mchezo uliopita Uwanja wa Stamford Bridge, The Blues wakishinda 4-0 dhidi ya Tottenham Machi 8, alishangilia kwa kushika kibendera kama mkongojo na mkono mwingine kujishika kiuno huku ameinama kama kikongwe, kuonyesha yeye ni mtu mzima anayefanya vitu uwanjani.
Eto'o kulia akiwania mpira dhidi ya Felipe Melo wa Galatasaray
Eto'o amewadhihirishia wapenzi wa Chelsea kwamba Mourinho hakosei kumpanga yeye badala ya Fernando Torres.
Eto’o ni mchezaji babu kubwa ambaye Chelsea watamuhitaji ikiwa wanataka kuzipiku Atletico, Bayern, Barcelona, Real au PSG baada ya kupangwa kwa droo ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Naye ndiye sababu za Mourinho kutamba kwamba atafika Fainali ya Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Estadio da Luz on Mei 24.
0 comments:
Post a Comment