Na Prince Akbar, Namibia
LICHA ya kutokuwepo kwa nyota kadhaa wa Taifa Stars katika mechi ya kirafiki dhidi ya Brave Warriors ya Namibia, timu hiyo imepania kuwafunga wenyeji wao katika mechi ya kirafiki itakayopigwa katika Uwanja wa Sam Nujoma, Jijini Windhoek Namibia.
Akizungumza mara baada ya kuwasili Windhoek kocha wa mpito wa Taifa Stars, Salum Madadi amesema wachezaji Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto hawatajiunga na kikosi hicho kutokana na tatizo la usafiri.
Hii inatokana na ndege za kuwawezesha kufika kwa muda mwafaka na pia kuwarusisha vilabuni kwao kwa muda unaotakiwa kukosekana kwa kuwa wachezaji hao wanatakiwa kujiunga na wenzao saa 48 kabla ya mchezo jambo ambalo lisingewezenana kwa watatu hao.
“Tumewasili salama na wachezaji wote wapo salama kiafya na wana ari ya mchezo,” alisema Madadi ambaye pia ni Mkurugenzi wa ufundi wa TFF na kuongeza kuwa hii pia itakuwa nafasi nzuri ya wachezaji walio kikosini kuonesha uwezo wao.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager imewasili ikiwa na wachezaji 15.
Wachezaji ambao walishindwa kusafiri kutoka Dar es Salaam ni pamoja na Edward Charles na Hassan Mwasapili ambao hati zao za kusafiria zilikuwa hazijakamilika.
Wachezaji ambao wamewasili Jijini Windhoek ni Shaban Kado, Mwadin Ally, Erasto Nyoni, Abdi Hassani Banda, nahodha Agrey Moris na Said Morad.
Wengine katika msafara huo unaoongozwa na Mjumbe wa Kanda ya Simiyu na Shinyanga, Epaphra Swai ni pamoja na Himid Mao, Amri Kiemba, Ramadhani Singano, Haruna Chanongo, Athanas Mdamu, Juma Luizio, Jonas Mkude na Mcha Khamis Mcha.
Mbali na wachezaji lakini pia timu hiyo imeambatana na kocha msaidizi Hafidh Badru, Mjumbe Ahmed Mgoyi, Daktari wa timu Juma Mwankemwa, Meneja wa timu, Boniface Clemence.
Baada ya kuwasili Taifa Stars ilifanya mazoezi mepesi ya kupasha misuli na leo Jumanne asubuhi ikafanya mazoezi katika Uwanja wa Sam Nujoma ambako mechi hii itapigwa.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema wao kama wadhamini wanatarajia ushindi mkubwa ili kuipandisha Tanzania katika viwango vya FIFA. Huu ni mwaka wa pili tangu Kilimanjaro Premium Lager ianze kuidhamini Taifa Stars na imewekeza zaidi ya Dola Milioni mbili kila mwaka.

0 comments:
Post a Comment