// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SPURS YABUTULIWA 3-1 NYUMBANI EUROPA LEAGUE NA BENFICA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SPURS YABUTULIWA 3-1 NYUMBANI EUROPA LEAGUE NA BENFICA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 14, 2014

    SPURS YABUTULIWA 3-1 NYUMBANI EUROPA LEAGUE NA BENFICA

    KLABU ya Tottenham Hotspur imeanza vibaya hatua ya 16 Bora ya Europa League baada ya usiku wa jana kuchapwa mabao 3-1 nyumbani Uwanja wa White Hart Lane, London na Benfica ya Ureno.
    Ni pigo lingine kwa Waingereza wa England baada ya Manchester City na Arsenal kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Spurs wanachungulia mlango wa kutokea kwenye michuano hiyo ya Ulaya.
    Spurs sasa inatakiwa kufanya maajabu ambayo yamewashinda City na Arsenal kwenda kushinda ugenini mabao 3-0 ili kusonga mbele.
    Mabao ya Wareno yalifungwa na Rodrigo dakika ya 30, Luisao dakika ya 58 na 84 wote pasi za Ruben Amorim, wakati bao la Spurs lilifungwa na Eriksen dakika ya 64.
    Katika mechi nyingine jana, Valencia iliifunga 3 – 0 Ludogorets, Napoli ilifungwa 1-0 nyumbani na Porto, Basel ililazimishwa sare ya bila kufungana na Salzburg nyumbani, Anzhi ilifungwa 1-0 nyumbani na AZ, Viktoria Plzen imefungwa 4-1 nyumbani na Olympique Lyon, Fiorentina imetoka sare ya 1 – 1 na Juventus na Real Betis imeilaza 2 – 0 Sevilla.
    Anaitazama: Rodrigo akiifungia Benfica Uwanja wa White Hart Lane jana
    Great start: The former Bolton forward celebrates his goal in front of the home fans
    Mwanzo mzuri: Mshambuliaji wa zamani wa Bolton akishangilia mbele ya mashabiki wa Spurs
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SPURS YABUTULIWA 3-1 NYUMBANI EUROPA LEAGUE NA BENFICA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top