KLABU kongwe Tanzania, Simba SC mwishoni mwa wiki ilifanya marekebisho ya Katiba yake katika Mkutano uliofanyika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay mjini Dar es Salaam.
Katika Mkutano huo, ulioongozwa na Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage wanachama walifanyia marekebisho ibara ya 26 (5 ) ya Katiba inayohusu sifa za wagombea.
Awali, kipengele hicho kilikuwa kinasomeka “Asiwe aliyewahi kutiwa hatiani kwa kosa la jinai kwa kuhukumiwa kifungo na baada ya marekebisho kitakuwa kinasomeka; “Asiwe ametiwa hatiani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita bila mbadala wa adhabu. Na endapo ametiwa hatihani kwa kifungo cha zaidi ya miezi sita, awe amemaliza muda wa miaka 5, tangu kuisha kwa kifungo husika bila kutiwa hatiani kwa kosa lingine lolote la jinai,”.
Aidha, wanachama wa Simba SC walifanyia marekebisho pia ibara ya 26 (9) katika sifa hizo hizo za wagombea, kinachosema awe ametimiza angalau miaka mitatu ya uanachama na sasa kitasomeka angalau awe na mwaka mmoja wa uanachama.
Ibara ya 25 (8) (iii) nayo imeboreshwa pia na sasa itasomeka; “Wajumbe watano wa Kamati ya Utendaji. Mwenyekiti aruhusiwe kuteua Wajumbe wengine watano wa Kamati ya Utendaji ambao anaweza kuwabadilisha kwa kadri anavyoona inafaa. Wajumbe hawa wa kuteuliwa wanatakiwa kuwa na sifa zili zile wanazotakiwa kuwa nazo Wajumbe wa kuchaguliwa na wanachama,”.
Baada ya Mkutano huo, Sekretarieti ya klabu hiyo sasa itakamilisha zoezi la marekebisho ya Katiba hiyo tayari kuanza kwa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo, uliopangwa kufanyika Mei 4, mwaka huu.
Mapema Jumamosi, siku moja kabla ya Mkutano wa marekebisho ya Katiba, Kamati ya Utendaji ya Simba SC ilipanga Mei 4, mwaka huu iwe tarahe ya Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo.
Pamoja na hayo, katika kikao chake, Kamati hiyo ya Utendaji pia iliunda Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti Damas Ndumbaro na Makamu wake, Salum Madenge, Katibu Issa Batenga, Katibu Msaidizi Khalid Kamguna na Wajumbe Kassim Dewji, Juma Simba na Amin Bakhresa.
Simba SC sasa inakabiliwa na wajibu wa kujipanga upya baada ya kupitia miaka mitatu migumu chini ya uongozi wa sasa wa Alhaj Ismail Aden Rage.
Migogoro, vita, ugomvi na matokeo mabaya katika mechi zake yaliyosababisha timu hiyo kufanya vibaya kwenye mashindano ndiyo yamekuwa maisha ya Simba SC kwa miaka ya karibuni.
Fedha nyingi zimekuwa zikitumika katika kusajili wachezaji wazuri pamoja na makocha, lakini wamekuwa hawadumu kwa kufukuzwa, au kuondoka baada ya muda mfupi kutokana na matokeo mabaya.
Yote imesababishwa na kukosekana utulivu ndani ya klabu, hali ambayo iliondoa umakini katika usimamizi wa timu na nguvu nyingi kuelekezwa katika mapambano ya migogoro.
Rage ametumia muda wake mwingi kupambana na wapinzani wake badala ya kushughulikia ustawi wa timu na hata mamilioni aliyokuwa anatumia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe kusajili na kuajiri makocha hayakuwa na manufaa.
Ndiyo, fedha alizotoa Poppe kusajili zimeteketea kwa moto tu, kwani imeshuhudiwa wachezaji wakisajiliwa kwa fedha nyingi, lakini baada ya muda mfupi sana wanavunjiwa mikataba na kulipwa fedha nyingi pia ili waondoke.
Hiyo imetokea kwa wachezaji kama Daniel Akuffo kutoka Ghana, Komabil Keita wa Mali, Paschal Ochieng wa Kenya na wengineo, wakiwemo hata wazawa.
Hakukuwa na umakini tena katika suala la kuongoza na kusimamia klabu, zaidi viongozi walielekeza nguvu zao kwenye mapambano baina yao.
Kocha Mserbia Milovan Cirkovick alilipwa fedha nyingi baada ya kuvunjiwa Mkataba kama ilivyokuwa kwa kocha Mfaransa, Patrick Liewig na hata mzalendo Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’.
Kwa ujumla hali haikuwa shwari Simba SC na kilichobaki ilikuwa bora tu timu iendelee kuwepo na kucheza mashindano, lakini hata umoja ulitoweka.
Matokeo yake sasa, mwakani Simba SC inaelekea kukosa nafasi ya kucheza michuano ya Afrika kwa mara ya pili mfululizo kutokana na kuzidiwa kete na Yanga na Azam.
Wazi, huu ni wakati wa Simba SC kujipanga upya na wenye jukumu la kuhakikisha klabu inajipanga upya ni wenye dhamana ya kuchagua viongozi.
Yanga SC wamepitia kwenye kipindi kigumu wakati fulani, lakini hatimaye wapinzani wao hao walijipanga bila kujali kufungwa 5-0 lakini wapate viongozi ambao wanaona watawafaa.
Sasa na wanachama wa Simba SC ngoma iko uwanjani kwao, kusuka au kunyoa ni wao- lakini wajue mazingira ya kustarehe kupitia timu yao, au kuendelea kuteseka watayatengeneza wao kutokana na kile ambacho watapanda.
Simba SC inahitaji viongozi makini, weledi hususan katika masuala ya soka, ambao wamekwishadhihirisha mapenzi yao katika klabu yao.
Simba wa kweli hawezi kuibuka tu kutaka kugombea, lazima atakuwa na mchango kwenye klabu yake kabla ya kuomba ridhaa ya wanachama.
Hilo ni la kutazama kwa umakini sana, kwani kinapowadia kipindi cha uchaguzi, huibuka watu wengi, wengine wanataka nafasi hizo kwa maslahi yao binafsi na hao ndiyo huwa mafundi wa kutumia rushwa.
Jambo jepesi tu wanachama wa Simba SC wajiulize, hao wanaowahonga fedha ili wawachague, wanataka wakafanye biashara gani pale Msimbazi wakiingia madarakani ili kurudisha fedha zao?
Kwa nini wasingejitokeza mapema kuungana na akina Hans Poppe kuhangaikia ustawi wa timu na leo waje noti ‘nje nje’ kutaka madaraka Simba SC?
Wanachama wa Simba SC, haswa wale walio mstari wa mbele kama makada, ambao tumezoea kuwaita makomandoo, watumie vizuri kipindi hiki kuwapigia kampeni watu ambao watakuwa na faida na klabu baadaye, na si kuichimbia kaburi klabu yao kwa kuridhisha matumbo yao. Jumatano njema.

0 comments:
Post a Comment