Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
UONGOZI wa Simba umekanusha vikali mashabiki wake kuhusika na vurugu zilizotokea katika mpambano wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Yanga na Al Ahly uliochezwa mwishoni mwa wiki Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao ulimalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ulitawaliwa na vurugu kiasi kutoka kwa mashabiki kufuatia bao la Yanga lililofungwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambapo baadhi ya mashabiki waling’oa viti na kuanza kurushiana.
Baadhi ya watu walidai kuwa vurugu hizo zilifanywa na mashabiki wa klabu za Simba na Yanga lakini hata hivyo uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi wamekanusha vikali taarifa hizo wakidai kuwa mashabiki wao hawawezi kufanya hivyo kutokana na kutokuwa na maslahi na mchezo husika.
Ofisa Habari wa Simba, Asha Muhaji amesema leo katika taarifa yake kwamba, mashabiki wao hawawezi kufanya jambo hilo kwani mchezo huo ulikuwa ukiwahusu Yanga na Al Ahly na wala haukuwahusu kabisa Simba hivyo ni jambo la ajabu kuhusishwa kwa klabu yake katika tukio hilo.
“Sisi tunaamini waliofanya vile ni mashabiki wa Al Ahly kwani ndio waliokuwa wapinzani wa Yanga siku hiyo, kwanza inashangaza Simba tunahusikaje katika mechi tusiyokuwa na maslahi nayo, pia ikumbukwe uongozi wa Simba siku zote umekuwa ukipinga vitendo vya uvunjifu wa amani zikiwemo vurugu, sasa mtu anaposema Simba imehusika mimi nadhani wana agenda ya siri kutaka kuichafua klabu yetu,” alisema.
Akizungumzia kigezo cha wahusika kuvaa jezi zenye rangi nyekundu inayotumiwa na klabu yake alisema, si kweli Simba ndiyo inayotumia jezi zenye rangi nyekundu pekee.
“Ukiachilia mbali Al Ahly wenyewe, zipo pia timu nyingine hapa nyumbani zinazotumia rangi kama hiyo kama vile Coastal Union, Small Simba nk. ingawa simaanishi kama ndizo zilizohusika na tukio hilo hapana, nachotaka kusisitiza kuwa rangi si kigezo cha kumtuhumu mtu, ningependa Simba isihukumiwe kwa hilo”. Alisema.
Asha alisema klabu yake ilishawahi kukatwa fedha zaidi ya Sh Milioni 25 kwa kosa kama hilo mwaka jana huku wahusika wakiwa hawana ushahidi wa kutosha hivyo amezitaka mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na matukio kama hayo kabla ya kuamua kuziadhibu klabu kwa kigezo cha dhana tu.

0 comments:
Post a Comment