Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
SIMBA SC imeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liwe macho na mchezo mchafu unaotaka kufanywa na wapinzani wao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC na Azam kwa mshambuliaji wao Mrundi, Amisi Tambwe.
Mchezo gani huo? Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba magazeti yamekuwa yakiandika Yanga na Azam wanamtaka Tambwe, lakini ajabu hawajawahi kufuatwa na kiongozi yoyote wa klabu hizo.
Poppe amesema kwamba kwa mujibu wa sheria za usajili, klabu yoyote inayomtaka mchezaji ambaye bado ana Mkataba na klabu yake, inatakiwa kwanza kuwasiliana na klabu yake na Tambwe amebakiza mwaka mmoja na ushei katika Mkataba wa miaka miwili aliosaini Agosti mwaka jana.
“Ingekuwa mkataba wake umebakiza miezi sita na hajaongezewa mwingine, basi klabu nyingine zingeruhusiwa kuzungumza naye, ila huyu mchezaji atamaliza mwaka wa kwanza wa Mkataba wake Agosti mwaka huu.
Kwa hivyo unaweza kuona ni kosa kwa kiongozi wa klabu yeyote kujaribu kufanya naye mazungumzo ya kumshawishi na kanuni za adhabu zipo, sasa sisi tunaiomba TFF iwe makini na mchezo wowote mchafu unaotaka kufanywa na wapinzani wetu,”alisema Poppe akiwa safarini kuelekea Japan jana kwa shughuli zake za kibiashara.
Alipoulizwa kama iwapo watapelekewa ofa na moja ya wapinzani wao hao katika Ligi Kuu, Poppe alisema watakuwa tayari kuwasikiliza, ila akawaambia kabisa dau la kuanzia la mauzo ya mchezaji huyo ni dola za Kimarekani 350,000.
“Ndiyo, sisi hatushuki chini, Okwi (Emmanuel) tulimuuza dola 300,000 Etoile du Sahel (ya Tunisia), hivyo na Tambwe hatuwezi kumuuza chini ya bei hiyo, atakayefika bei tutampa huyo mchezaji, sisi tutaleta mkali mwingine,”alisema Poppe.
Hadi sasa, Tambwe amekwishaichezea Simba SC mechi 23 katika mashindano yote na kuifungia mabao 19, kati ya hayo 17 amefunga katika Ligi Kuu na kumfanya aongoze kwenye mbio za ufungaji bora kwa mabao manne zaidi dhidi ya Kipre Tchetche wa Azam anayemfuatia.
Okwi aliuzwa Tunisia, lakini hadi sasa Simba SC haijalipwa fedha zake na Etoile, wakati mchezaji huyo alivurugana na klabu hiyo akidai alikuwa halipwi mishahara, hivyo kufungua kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
FIFA ilimruhusu kujiunga na timu nyingine wakati kesi yake ikiendelea naye akaenda SC Villa ya kwao,Uganda kabla ya Desemba mwaka jana kutua Yanga SC anakoendelea na kazi hivi sasa.
Wakati Simba SC inadai fedha zake Etoile, klabu hiyo ya Tunisia nayo imefungua kesi mpya FIFA, safari hii ikitaka kulipwa fidia ya Euro Milioni 1.5 sawa na Sh. Bilioni 3.1 za Tanzania.
SIMBA SC imeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liwe macho na mchezo mchafu unaotaka kufanywa na wapinzani wao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC na Azam kwa mshambuliaji wao Mrundi, Amisi Tambwe.
Mchezo gani huo? Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba magazeti yamekuwa yakiandika Yanga na Azam wanamtaka Tambwe, lakini ajabu hawajawahi kufuatwa na kiongozi yoyote wa klabu hizo.
Anawatoa udenda; Amisi Tambwe inadaiwa Yanga SC na Azam FC zinamtaka wakati bado ana Mkataba na Simba SC |
Poppe amesema kwamba kwa mujibu wa sheria za usajili, klabu yoyote inayomtaka mchezaji ambaye bado ana Mkataba na klabu yake, inatakiwa kwanza kuwasiliana na klabu yake na Tambwe amebakiza mwaka mmoja na ushei katika Mkataba wa miaka miwili aliosaini Agosti mwaka jana.
“Ingekuwa mkataba wake umebakiza miezi sita na hajaongezewa mwingine, basi klabu nyingine zingeruhusiwa kuzungumza naye, ila huyu mchezaji atamaliza mwaka wa kwanza wa Mkataba wake Agosti mwaka huu.
Kwa hivyo unaweza kuona ni kosa kwa kiongozi wa klabu yeyote kujaribu kufanya naye mazungumzo ya kumshawishi na kanuni za adhabu zipo, sasa sisi tunaiomba TFF iwe makini na mchezo wowote mchafu unaotaka kufanywa na wapinzani wetu,”alisema Poppe akiwa safarini kuelekea Japan jana kwa shughuli zake za kibiashara.
Alipoulizwa kama iwapo watapelekewa ofa na moja ya wapinzani wao hao katika Ligi Kuu, Poppe alisema watakuwa tayari kuwasikiliza, ila akawaambia kabisa dau la kuanzia la mauzo ya mchezaji huyo ni dola za Kimarekani 350,000.
“Ndiyo, sisi hatushuki chini, Okwi (Emmanuel) tulimuuza dola 300,000 Etoile du Sahel (ya Tunisia), hivyo na Tambwe hatuwezi kumuuza chini ya bei hiyo, atakayefika bei tutampa huyo mchezaji, sisi tutaleta mkali mwingine,”alisema Poppe.
Tahadhari; Hans Poppe amezionya Yanga na Azam zisithubutu kuzungumza na Tambwe, wakifanya hivyo watakuwa wamevunja sheria za usajili na ameiomba TFF iwe macho dhidi ya mchezo mchafu |
Okwi aliuzwa Tunisia, lakini hadi sasa Simba SC haijalipwa fedha zake na Etoile, wakati mchezaji huyo alivurugana na klabu hiyo akidai alikuwa halipwi mishahara, hivyo kufungua kesi Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
FIFA ilimruhusu kujiunga na timu nyingine wakati kesi yake ikiendelea naye akaenda SC Villa ya kwao,Uganda kabla ya Desemba mwaka jana kutua Yanga SC anakoendelea na kazi hivi sasa.
Wakati Simba SC inadai fedha zake Etoile, klabu hiyo ya Tunisia nayo imefungua kesi mpya FIFA, safari hii ikitaka kulipwa fidia ya Euro Milioni 1.5 sawa na Sh. Bilioni 3.1 za Tanzania.
0 comments:
Post a Comment