// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC WAIFUATA PRISONS KWA 'PIPA' KESHO MBEYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC WAIFUATA PRISONS KWA 'PIPA' KESHO MBEYA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 06, 2014

    SIMBA SC WAIFUATA PRISONS KWA 'PIPA' KESHO MBEYA

    Na Baby Akwitende, Dar es Salaam
    KOCHA Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic, amesema ataondoka na wachezaji 18 kesho kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Prisons utakaofanyika Jumapili.
    Simba SC itaondoka kwa ndege ya Fast Jet, lakini wachezaji watakaokuwemo kwenye msafara hao watajulikana baada ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kilichokuwa Namibia kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa na wenyeji wao jana kutua nchini kesho mapema.
    Sisi tuko poa tu; Kocha Mkuu wa Simba SC, Zdravko Logarusic kushoto akiwa na Msaidizi wake, Suleiman Matola kulia. Kesho wanakwenda Mbeya kwa ndege

    Stars ilitoka sare ya 1-1 na Namibia jana Uwanja wa Sam Nujoma mjini Windhoek na Logarusic anasubiri wachezaji wake waliokuwa kwenye kikosi hicho kama wote wako fiti na hakuna majeruhi, basi atawajumuisha kwenye safari ya Mbeya. 
    Simba na Prisons zitamenyana Jumapili kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kuanzia saa 10:00 jioni, katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua.
    Zdravko ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba timu yake iko vizuri kuelekea mchezo na maafande hao wa jeshi la Magereza na ana matumaini ya ushindi.
    Mshambuliaji Amisi Tambwe anayeongoza kwa mabao Ligi Kuu akiwa amefunga 19 hadi sasa, naye anatarajiwa kurejea leo kutoka Burundi tayari kwa safari ya Mbeya kwenda kujaribu kuongeza idadi yake ya mabao.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA SC WAIFUATA PRISONS KWA 'PIPA' KESHO MBEYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top