// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SI JAMBO JEPESI KUMTOA AL AHLY KWA MTAJI WA USHINDI WA 1-0 NYUMBANI, YANGA SC WAJIPANGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SI JAMBO JEPESI KUMTOA AL AHLY KWA MTAJI WA USHINDI WA 1-0 NYUMBANI, YANGA SC WAJIPANGE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 02, 2014

    SI JAMBO JEPESI KUMTOA AL AHLY KWA MTAJI WA USHINDI WA 1-0 NYUMBANI, YANGA SC WAJIPANGE

    YANGA SC jana imeandika historia mpya, baada ya kuifunga bao 1-0 Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kwanza wa kuwania kucheza Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Shukrani kwake, beki na Nahodha Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 83 akimalizia kona maridadi ya winga Simon Msuva kutoka wingi ya kulia.
    Kona hiyo ilitokana na kipa Sherif Ekram Ahmed kupangua shuti kali la mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi. 
    Yanga SC kwa ujumla jana walicheza vizuri na wangeweza kutoka uwanjani na ushindi mnene, kama wangetumia vyema nafasi zao nzuri walizotengeneza pasipo kukosa mabao zaidi ya matatu ya wazi.

    Simon Msuva alikuwa chanzo kizuri cha mashambulizi ya Yanga upande wa kulia, lakini Waganda Emannuel Okwi na Hamisi Kiiza walishindwa kutumia nafasi.
    Haruna Niyonzima, Frank Domayo na Mrisho Ngassa kwa pamoja walicheza vizuri katika safu ya kiungo kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili, Ngassa alishambulia kutokea pembeni zaidi baada ya kuingia kwa Didier Kavumbangu kuchukua nafasi ya Kiiza.
    Kipindi cha pili, Ahly kidogo walibadilika na kuongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Amr Gamal, ambaye hata hivyo alidhibitiwa vikali na walinzi wa Yanga, ambao jana walicheza kwa umakini wa hali ya juu.
    Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mholanzi Hans van der Pluijm, kumuingiza mshambuliaji Didier Kavumbangu kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza yaliongeza makali ya safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
    Kavumbangu aliwapa wakati mgumu mno mabeki wa Ahly tangu alipoingia dakika ya 66 hata mashabiki wa Yanga wakatamani angekuwa uwanjani tangu mwanzo.  
    Pamoja na kufungwa 1-0, Al Ahly inayofundishwa na kocha Mohamed Yousef, ilionyesha upinzani kwa Yanga SC, jambo ambalo linaashiria katika mchezo wa marudiano lolote linaweza kutokea.
    Baada ya matokeo haya, Yanga SC sasa inahitaji sare ya ugenini au kufungwa kwa tofauti ya bao moja mfano 2-1 au 3-2 ili wasonge mbele hatua ya 16 Bora kwa faida ya bao la ugenini.
    Kihistoria hii inakuwa mara ya kwanza kabisa Yanga SC inapata ushindi dhidi ya timu ya Misri na Kaskazini mwa Afrika kwa ujumla, kwani mara zote imekuwa ikifungwa na kutoa sare.
    ‘Bismillah’ Yanga inakutana kwa mara ya kwanza na Al Ahly na timu za Kaskazini kwa ujumla ilikuwa ni mwaka 1982 katika Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa na katika mchezo wa kwanza mjini Cairo, Waarabu hao walishinda 5-0 na marudiano Dar es Salaam timu hizo zikatoka sare ya 1-1. 
    Zikakutana tena mwaka 1988 katika Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa mchezo wa kwanza ukimalizika kwa sare ya bila kufungana Dar es Salaam wakati marudiano mjini Cairo, Yanga wakabebeshwa 4-0. 
    Mara ya mwisho Yanga kukutana na Ahly kabla ya jana ilikuwa mwaka 2009 katika Raundi ya Kwanza pia Ligi ya Mabingwa pia na mchezo wa kwanza Cairo, wakafungwa 3-0 wakati marudiano Dar es Salaam wakafungwa pia 1-0.
    Historia imeandikwa, Machi 1, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga SC wamepata ushindi wa kwanza kabisa dhidi ya Ahly na timu za Kaskazini kwa ujumla na Machi 8 Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, Misri Yanga watajaribu kuitoa mashindanoni kwa mara ya kwanza kabisa timu ya Kaskazini mwa Afrika tangu ianze kukutana nazo 1982.
    Yanga SC mwaka huu inaonyesha kudhamiria kuvunja mwiko wa kunyanyaswa na Ahly na timu za Kaskazini mwa Afrika kwa ujumla- kutokana na aina ya maandalizi yake.
    Mapema Januari ilikwenda kuweka kambi ya karibu wiki mbili mjini Antalya, Uturuki na pamoja na mazoezi makali, ilipata mechi nne za kujipima nguvu dhidi ya timu za Ulaya na kushinda mbili na kutoa sare mbili.
    Ikumbukwe Desemba mwaka jana Yanga SC ilivunja benchi lake zima la Ufundi, ikiwaondoa Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts na Wasaidizi wake Freddy Felix Minziro na Razack Ssiwa na kuwaajiri Mholanzi mwingine, Hans van der Pluijm na Wasaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa na Juma Pondamali.
    Ilibadilisha hadi Daktari wa timu,  ikmpiga chini Nassor Matuzya na kumuajiri Juma Sufiani.  
    Tangu imerejea kutoka Uturuki, Yanga SC haijapoteza mechi hata moja katika Ligi Kuu ikishinda mbili nyumbani na kutoka sare moja ugenini, wakati katika Ligi ya Mabingwa, iliitoa Komorozine ya Comoro kwa jumla ya mabao 12-0, ikishinda 7-0 nyumbani na 5-2 ugenini.
    Hii inaashiria kwamba Yanga SC ya mwaka huu ni tofauti kidogo na Yanga zile ambazo Al Ahly imezoea kukutana nazo miaka ya nyuma.
    Al Ahly ilileta wawakilishi wake mwezi huu kuja kuitazama Yanga ikimenyana na Komorozine Dar es Salaam na mabingwa hao wa Bara nao wakampeleka kocha wao Msaidizi, Charles Boniface  Mkwasa kwenda kuwatazama Waarabu hao wakimenyana na CS Sfaxien ya Tunisia wiki iliofuata katika mechi ya Super Cup mjini Cairo.
    Yanga SC imekuwa kambini Bagamoyo tangu imerejea kutoka Uturuki, na imekuwa ikitokea huko kwenda kwenye mechi zake zote na kurejea huko huko kabla ya mapema wiki hii kuhamia katika hoteli ya Bahari Beach kwa ajili ya maandalizi na Al Ahly.
    Inaonekana ni kiasi gani Yanga SC chini ya Mwenyekiti wake, Bilionea Yussuf Manji imedhamiria kufanya mapinduzi. 
    Yanga SC sasa wanatakiwa kusahau ya jana na kujipanga kwa ajili ya mchezo wa marudiano, ambao unatarajiwa kuwa mgumu zaidi kwao.
    Watarajie kufanyiwa hila na wapinzani wao, watakazofanikiwa kuona na ambazo hawatafanikiwa kuona- kikubwa waende Misri wakijua wanakwenda vitani.
    Si jambo jepesi kuitoa timu ya Misri au Kaskazini mwa Afrika kwa mtaji wa ushindi wa 1-0 nyumbani- Simba SC waliifunga Haras El Hodoud 2-1 Dar es Salaam wakaenda kupigwa 5-0 Alexandrie. 
    Yanga SC wasilewe sifa hata chembe, wajiandae kwenda kumalizia vizuri kazi waliyoianza jana Uwanja wa Taifa. Hongera Yanga SC na kila la heri kuelekea mchezo wa marudiano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SI JAMBO JEPESI KUMTOA AL AHLY KWA MTAJI WA USHINDI WA 1-0 NYUMBANI, YANGA SC WAJIPANGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top