Na Renatus Mahima, Dar es Salaam
KLABU ya Yanga SC imesitisha mpango wake wa kuandamana kuishinikiza serikali kuwapa eneo la ziada na kibgali cha kujenga uwanja wa kisasa baada ya uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuahidi kuyafanyia kazi maombi yao.
Alhamisi ya wiki iliyopita, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali aliipa serikali siku tano ambazo zilimalizika jana kuhakikisha unatoa idhini ya kujenga uwanja wa kisasa katika eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam huku ukitishia kufanya maandamano endapo usingetekelezewa hitaji hilo.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga mjini hapa mchana wa leo, Akilimali amesema wameamua kusitisha mpango wao wa kuandamana baada ya uongozi wa Halmashauri ya Ilala na mkoa wa Dar es Salaam kuahidi kuyafanyia kazi mapendekezo yao.
"Kama tulivyosema wiki iliyopita, tulipanga kufranya maandamano ili kuondoa kauzibe ambako tuliona tulikuwa tunafanyiwa na baadhi ya watendaji wa serikali. Lakini tumeamua kusitisha mpango huo kwa sababu serikali imesikia kilio chetu na imeahidi kuyafanyia kazi maombi yetu," amesema Akilimali.
"Jana uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Francis Kifukwe, mimi (Akilimali), Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Yanga, Bakili Makele na viongozi wengine wengi wa Yanga tulikutana na Meya wa Ilala (Jery Slaa) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (Said Meck Sadick) wakatuahidi suala letu litashugulikiwa kwa kufuata taratibu za serikali," amesema Akilimali huku akikataa kuweka wazi muda waliopewa na serikali kabla ya kutolewa kwa kibali hicho.

Hatuandamani tena; Mzee Akilimali kushoto akizungumza leo Jangwani |

0 comments:
Post a Comment