// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SABABU KWA NINI AZAM TV HAITARUSHA PAMBANO LA YANGA NA AL AHLY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SABABU KWA NINI AZAM TV HAITARUSHA PAMBANO LA YANGA NA AL AHLY - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 01, 2014

    SABABU KWA NINI AZAM TV HAITARUSHA PAMBANO LA YANGA NA AL AHLY

    "Tumepokea maswali na simu nyingi sana zikiuliza kama Azam TV itaonesha mechi kati ya Yanga na Al Ahal leo, jibu ni kwamba HAPANA... 
    ukweli ni kwamba tulipokea maombi toka kwa agent aliyenunua pambano kwa niaba ya Watu wa Misri ambaye aliomba Azam TV impe gharama za kuzalisha ili kuweza kupeleka feed yenye ubora wa kimataifa North Africa & Middle East na ikiwezekana kuonesha nchini Tanzania.
    Maji bora, mchezaji bora; Mshambuliaji tegemeo wa Al Ahly, Amr Gamal akinywa maji ya Uhai yanayozalishwa na kampuni ya Bakhresa Group Limited, wamiliki wa Azam TV jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati wa mazoezi ya timu hiyo 
    Katika vikao vyote na Agent Azam TV iliweka wazi kuwa ipo tayari kuzalisha bure na hata kama ikibidi kuonesha delayed sawa kwa kuwa Yanga walionesha wazi kuzuia Live Coverage nchinikwa kuhofia mapato kupungua. 

    Bahati mbaya Yanga waliikataa Azam TV na kuamua kutoa pesa waliyolipwa kukilipa kituo kimoja nchini ambacho ndicho kilichopewa kandarasi kwa malipo licha ya kutokidhi vigezo vya watu wa Egypt ambao walitaka angala 8 Camera OB na Azam TV iliwapa 10 Camera OB with HD Feed
    Kwa taarifa hii tungependa kuwaarifu wateja wetu kuwa Azam TV ilikuwa tayari kuwapa Yanga na Agent ushirikiano wote ili pesa yote waliyopewa na Watu wa Misri iingie klabuni lakini wao wameamua kuitumia kulipia production iliyo sub-standard ili mradi tuu kuinyima fursa Azam TV
    Pamoja na haya yote Azam TV inaitakia kila la kheri klabu ya Yanga kwenye mchezo wake wa leo, na inaamini matatizo hayapo kati ya Azam na Yanga kama taasisi bali mtu mmoja mwenye nguvu ndani ya Yanga,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SABABU KWA NINI AZAM TV HAITARUSHA PAMBANO LA YANGA NA AL AHLY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top