MSHAMBULIAJI Wayne Rooney usiku huu amekumbushia enzi za David Beckham alipoifungia bao la umbali wa mita 58 Manchester United ikiifunga West Ham mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Upton Park.
Akirejea katika Ligi Kuu baada ya kufanikiwa kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuitoa Olympiacos ya Ugiriki, mwanasoka huyo wa kimataifa wa England aliifungia mabao mawili timu ya David Moyes dakika ya nane na 73 na kuiwezesha kubeba pointi tatu.
Bao la pili la Rooney limemfanya atimize mabao 212 na kumfikia Jack Rowley katika nafasi ya tatu ya ufungaji bora wa kihistoria Man United, lakini ni bao lake la kwanza alilofunga dakika ya nane ambalo litabakia katika kumbukumbu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alifunga bao la ajabu, akikumbushia bao alilofunga Beckham dhidi ya Wimbledon mwaka 1996. United sasa inatimiza pointi 51 baada ya mechi 30, ingawa inabaki nafasi ya saba, ikizidiwa pointi mbili na Tottenham Hotspur iliyo nafasi ya sita.
Bao ambalo halitasahaulika: Rooney amefunga bao kutoka umbali wa mita 57.9 Uwanja wa Upton Park usiku huu
Wayne Rooney baada ya kufutumua shuti la mbali
Pongezi: Wachezaji wa United wakimpongeza Rooney baada ya bao la kwanza
0 comments:
Post a Comment