MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ameonyesha moyo wa kibinadamu kwa kutoa ofa ya kugharamia matibabu ya mtoto wa umri wa meizi 10 anayesumbuliwa na ugonjwa wa mishipa ya fahamu.
Erik Ortiz Cruz anaanguka hadi mara 30 kwa siku kuyokana na ugonjwa wa kifafa na upasuaji ndio suluhisho pekee la hali yake.
Faimili ya mtoto huyo haina uwezo wa kulipa gharama za matibabu hospitali ambayo kila kipimo peke kinagharimu kiasi cha Pauni 5,020 na gharama za upasuaji ni Pauni 50,240.
Muungwana: Cristiano Ronaldo ametoa zaidi ya Pauni 50,000 kwa upasuaji wa mtoto wa umri wa miezi 10, Erik Ortiz Cruz
Mtoto mwenyewe ni huyu: Erik Ortiz Cruz akiwa na mama yake hospitali
0 comments:
Post a Comment