REAL Madrid imegawana pointi na jirani zao Atletico baada ya kufungana mabao 2-2 atika mchezo wa La Liga usiku wa jana, hivyo kufanya mbio za ubingwa ziendelee kuwa farasi watatu pamoja na Barcelona.
Sifa zimuendee refa Carlos Ferreiro aliyeumudu mchezo mkali na uliokuwa na upinzani wa hali ya juu. Alikuwa ni Cristiano Ronaldo aliyeinusuru Real kulala kwa bao la dakika ya 82 na kufanya Real imalize miaka 15 ya kuchezwa bila kufungwa kwenye Uwanja wa wapinzani hao wa Jiji.
Madrid imeshinda mechi 12 na kutoa sare mbili tangu Atletico iliposhinda dhidi yao mara ya mwisho nyumbani mwaka 1999. Real ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao jana mfungaji Benzema dakika ya tatu na Koke akawasawazishia wenyeji dakika ya 28 kabla ya Gabi kuwafungia la pili dakika ya 45, lakini Ronaldo akainusuru Real kuzama dakika ya 82.
Real inaendelea kuongoza La Liga kwa pointi zake 64 baada ya kucheza mechi 26, ikifuatiwa na Barcelona pointi 63 mechi 26 pia, wakati Atletico ni ya tatu pointi 61 mechi 26 pia.
0 comments:
Post a Comment