MAHAKAMA ya Ujerumani imemhukumu rais wa Bayern Munich – Mabingwa wa soka barani Ulaya, Uli Hoeness kifungo cha miaka mitatu na miezi sita jela kwa kukwepa kodi.
Uli Hoeness alikiri kukwepa kodi ya mamilioni ya Euro.
Rais huyo mwenye umri wa miaka 62 ambaye alikuwa mshambuliaji wa kikosi cha Ujerumani Magharibi kilichotwaa kombe la dunia mwaka 1962 aliweka mamilioni hayo kwenye akaunti yake ya siri kwenye benki ya Uswisi.
Wanasheria wake walisema mteja wao anastahili kukwepa adhabu kwa sababu alikiri mwenyewe juu ya ukwepaji huo wa kodi. Lakini majaji wakasema kuungama kwake hakuzuii sheria kuchukua mkondo wake.
Waendesha mashitaka wakapigilia msumari kuwa aliungama baada ya kugundua kuwa tayari uchunguzi umeanza.
Alituhumiwa kukwepa kodi ya euro 3.5 sawa na pauni milioni 2.9 lakini baadae akikiri kukwepesha euro milioni 15 alizoweka Uswisi na hivyo jumla yake ikawa amekwepa kodi ya euro milioni 27.2.

Na uzee huu jela; Rais wa Bayern Munich atatumikia kifungo cha miaka mitatu na nusu |
Wanasheria wake walisema mteja wao anastahili kukwepa adhabu kwa sababu alikiri mwenyewe juu ya ukwepaji huo wa kodi. Lakini majaji wakasema kuungama kwake hakuzuii sheria kuchukua mkondo wake.
Waendesha mashitaka wakapigilia msumari kuwa aliungama baada ya kugundua kuwa tayari uchunguzi umeanza.
Alituhumiwa kukwepa kodi ya euro 3.5 sawa na pauni milioni 2.9 lakini baadae akikiri kukwepesha euro milioni 15 alizoweka Uswisi na hivyo jumla yake ikawa amekwepa kodi ya euro milioni 27.2.
Enzi zake; Uli Hoeness alikuwa mchezaji tegemeo Ujerumani enzi zake |
0 comments:
Post a Comment