// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PIUS NDIEFI SIELENU ANATULAZIMISHA TUUSIKILIZIE MCHAKATO HUU WA TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PIUS NDIEFI SIELENU ANATULAZIMISHA TUUSIKILIZIE MCHAKATO HUU WA TFF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 12, 2014

    PIUS NDIEFI SIELENU ANATULAZIMISHA TUUSIKILIZIE MCHAKATO HUU WA TFF

    JOPO maalum la watu 28 iliyoundwa kusaka vipaji katika mpango maalumu wa kuiboresha timu ya taifa, Taifa Stars inakutana Lushoto mkoani Tanga kwa siku saba kuanzia Machi 9, mwaka huu kwa ajili ya kupata orodha ya mwisho ya wachezaji waliopatikana.
    Yalifanyika mashindano maalum nchi nzima na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likawagawa wataalamu hao 28 katika vituo tofauti kutazama vipaji- na sasa wanakutana Lushoto kwa siku saba kutafuta orodha ya mwisho.
    Ni kwamba, majina yatakayopatikana wachezaji watawekwa kambini chini ya mwalimu mpya wa timu ya taifa anayekuja mwishoni wa mwezi huu kuandaliwa kuunda Taifa Stars mpya.

    Katika kikao hicho, wang’amua vipaji hao watapitia majina ya wachezaji walioteuliwa ikiwemo kuwaangalia tena kwenye video kwa vile mechi zote zilirekodiwa. Wachezaji watakaoteuliwa katika mpango huo baadaye wataingia kambini mkoani Mbeya.
    Wang’amua vipaji waliopo ni Abdul Mingange, Boniface Pawasa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.
    Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.
    Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Ayoub Nyenzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.
    Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa alikuwa Misri na timu yake na amerejea leo, ingawa bado haijafahamika kama atakwenda au la.
    Unaweza ukajiuliza, kwa nini TFF itumie njia ndefu namna hii kusaka wachezaji wa kuunda timu ya taifa, wakati nchi ina ligi kuanzia za mikoa hadi Ligi Kuu, ambako wang’amua vipaji wangeweza kwenda kufanya shughuli yao.
    Bado tuna mashindano mengi ya kuibua vipaji kama Airtel Rising Stars na Copa Coca Cola, lakini kwa nini watu watumie njia hii ndefu kusaka vipaji.
    Ni haki kabisa kuwa na mawazo kama hayo na wengine wanaweza wakasema huo ni ufujaji wa fedha chache ambazo shirikisho inazo, zisizotosha tu kukidhi mahitaji mengi muhimu ya soka yetu.    
    Lakini wakati mwingine, michakato mingine unaweza kuiacha iendelee ili uone mwisho wake kama unaweza kuzaa matunda au vipi.  
    Pius Ndiefi Sielenu alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon kilichocheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002 na Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2004.
    Pia alifunga bao la ushindi katika Nusu Fainali ya Kombe la Mabara mwaka 2003 Cameroon ikiitoa Colombia, katika mchezo ambao mchezaji mwenzake, Marc-Vivien Foe alifia uwanjani.
    Nakumbuka mchezaji huyu alipatikana baada ya mchakato kama huu ambao Tanzania inaufanya sasa. 
    Cameroon pamoja na kuwa na ligi nzuri zenye ushindani, idadi kubwa ya wachezaji wanaocheza Ulaya, lakini mwishoni mwa miaka ya 1990 walilazimika kuingia msituni kusaka vipaji vya kuboresha timu yao ya taifa na katika zoezi hilo miongoni mwa wachezaji waliopatikana ni Ndiefi.  
    Kweli, ukirejea kwenye uhalisia, kama nchi ina ligi na mashindano mengine ya kuvumbua vipaji, huwezi kuona mantiki ya kuingia gharama nyingine za fedha na muda eti kusaka vipaji nje ya mfuumo huo.
    Ila kwa kuzingatia baadhi ya historia kama ya Pius Ndiefi Sielenu, hatuna busi kuusikilizia huu mchakato. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PIUS NDIEFI SIELENU ANATULAZIMISHA TUUSIKILIZIE MCHAKATO HUU WA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top