KLABU ya Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake Jack Wilshere kuumia akiichezea timu ya taifa ya England dhidi ya Denmark jana usiku na atakuwa nje kwa wiki sita akipatiwa matibabu.
Kiungo huyo mahiri alikwenda chini baada ya kugongana na Daniel Agger kipindi cha kwanza katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Wembley na England kushinda 1-0 bao pekee la Danie Sturridge.
Pigo: Kiungo wa Arsenal na England, Jack Wilshere atakuwa nje kwa wiki sita baada ya kuumia jana
Muumizaji: Wilshere alianguka baada ya kugongana na beki wa Denmark, Daniel Agger mwanzoni mwa mchezo
Wilshere akiugulia maumivu baada ya kuumia
Pamoja na machela kuingizwa uwanjani, lakini Wilshere alikuwas tayari kuendelea na mchezo hadi dakika ya 59 alipompisha Adam Lallana.
Atakosa mechi ya Raundi ya sita ya Kombe la FA, Arsenal ikimenyana na Everton Jumapili, mechi ya marudiano na Bayern Munich Ligi ya Mabingwa Ulaya Hatua ya 16 Bora na mechi kadhaa za Ligi Kuu ya England zikiwemo dhidi ya Tottenham, Chelsea, Swansea City, Manchester City, Everton na West Ham.
Anaweza kuwa tayari kurejea uwanjani katika mchezo na Hull City Aprili 19 na kisha kuanza kupambana na kurudi katika kiwango chake kuwania nafasi ya kuwamo kwenye kikosi cha England kitakachokwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia katikati ya mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment