// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); PAUKWA, PAKAWA YA UJENZI WA UWANJA WA KISASA YANGA SC, NI... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE PAUKWA, PAKAWA YA UJENZI WA UWANJA WA KISASA YANGA SC, NI... - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Sunday, March 16, 2014

    PAUKWA, PAKAWA YA UJENZI WA UWANJA WA KISASA YANGA SC, NI...

    TAZAMA picha hiyo hapo chini, ni kikosi cha Yanga SC kikiwa katika Uwanja wa Kaunda mwaka 2005, uliopo makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kabla ya mechi moja ya kirafiki, siikumbuki.
    Yanga SC ilikuwa inautumia Uwanja wa Kaunda kwa mazoezi na mechi ndogo ndogo na kwa muda mrefu, viongozi mbalimbali wa klabu hiyo wamekuwa na mipango ya kuuendeleza, bila mafanikio.
    Ama wanawahadaa wanachama wao, au kweli wanakuwa na nia lakini wanakwamishwa kwa namna moja au nyingine.
    Mwaka 2000, rais wa Yanga SC Tarimba Abbas aliweka dhamira ya kuujenga Uwanja huo, ili wautumie kwa michezo ambayo haihusishi Simba na Yanga kwa imani kwamba utakidhi idadi ya mashabiki.
    Angalia umati; Kikosi cha mwaka 2005 kikiwa Uwanja wa Kaunda kabla ya mechi ya kirafiki 

    Lakini, kwa bahati mbaya Tarimba ambaye katika viongozi wa karibuni ndiye aliyeonekana kuwa na dhamira ya dhati ya kufanya hivyo, akajiuzulu mwaka 2002 baada ya kukerwa na uongozi wa Chama cha Soka Tanzania (FAT), sasa shirikisho (TFF).
    Chanzo ni mechi ya Machi 31, mwaka 2002 Yanga SC ikifungwa mabao 4-1 na mahasimu Simba SC katika fainali ya iliyokuwa michuano ya Kombe la Tusker.
    Mechi hiyo iliyohudhuriwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, chupuchupu ivunjike dakika ya 32, baada ya Madaraka Suleiman kufunga bao ambalo kabla ya kufumua shuti lililomshinda kipa Manyika Peter, aliushika mpira kwa makusudi, ili kuuweka sawa. 
    Tarimba aliinuka na kuwaonyesha ishara wachezaji wake watoke uwanjani na hapo ndipo meza kuu aliyokuwa ameketi mzee Mwinyi, ilipoanza kushambuliwa kwa chupa za maji na mashabiki wa Yanga. 
    Refa wa mchezo huo, Abdulkadir Omar alisubiri hadi vurugu zilipotulizwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ndipo akaendeleza mchezo. Tarimba alitoka nje na hakutaka kuendelea kushuhudia mchezo huo. 
    Baada ya hapo, alifungiwa na FAT- na kabla hajamaliza adhabu, akajiuzulu, akiamini anapigwa vita kwa misimamo yake.  
    Nitawakumbusha wafungaji wa siku hiyo, mabao ya Simba SC yalifungwa na Mkenya Mark Sirengo dakika ya tatu na 76, Madaraka Selemani dakika ya 32 na Emanuel Gabriel dakika ya 83, wakati la Yanga lilifungwa na Sekilojo Chambua dakika ya 16.
    Baada ya Tarimba wamepita Francis Kifukwe, Imani Madega na Lloyd Nchunga kama viongozi wakuu wa Yanga SC na wote walitoa ahadi siyo tu ya kuendeleza Uwanja wa Kaunda, bali hata jengo dogo la klabu hiyo liliopo Mtaa wa Mafia.
    Hata hivyo, hadi wanamaliza muda wao na sasa ameingia Yussuf Manji, bado Uwanja wa Kaunda hauwezi kutumika hata kwa mazoezi kwa sababu umeharibika zaidi.
    Yanga SC ilikuwa inaingiza fedha nyingi kwa viingilio vya watu kutazama maaozezi na hizo mechi na wakati huo ikiwa hauna ufadhili wala mikataba ya udhamini, zilisaidia mno kuchangia kuendesha timu.
    Matatizo ya kifedha Yanga SC yalipungua mwaka 2006 baada ya kujitokeza Manji, aliyeanza kama mfadhili kwani amekuwa akitoa fedha zake kuendesha timu na hata wapenzi na wanachama wa timu hiyo wamesahau umuhimu wa kuuendeleza Uwanja wa Kaunda.
    Manji pia alipoingia madarakani alionyesha dhamira ya kuuendeleza Uwanja wa huo, tena akiahidi kujenga Uwanja wa kisasi na akatoa hadi ramani, lakini kilichofuata baada ya hapo ni sababu za kwa nini zoezi linakwama.
    Kuna wakati ilielezwa Hati za majengo yote ya Yanga SC hazionekani, zipo mikononi mwa watu zikiwa na majina yao binafasi, hivyo inakuwa ngumu kufanya jambo lolote.
    Baadaye wakasema mzee mwenye hati za Yanga alipatikana, lakini haijaelezwa hadi leo kama amezikabidhi kwa wahusika au la, maana hakuna asiyejua mali hizo ni za Yanga.   
    Wiki hii, waliibuka Wazee wa klabu hiyo wakisema wanaipa siku tano Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam kutoa idhini ya kujenga Uwanja wa kisasa katika eneo la Jangwani mjini hapa, vinginevyo wataandamana kushinikiza suala hilo.
    Akizungumza na Waandishi wa Habari makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Jangwani na Twiga, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali alisema wamebaini wanawekewa vikwazo na baadhi ya madiwani wa Manispaa hiyo.
    “Jana kulikuwa na kikao cha baraza la madiwani na Yanga tuliomba tuhudhurie kikao hicho kwa sababu moja ya ajenda ilikuwa ombi letu la kuongezwa eneo na kibali cha ujenzi wa Jangwani City. Cha kusshangaza tulikatazwa kuingia kwenye kikao hicho na kukalishwa nje ya ukumbi kwa saa 10,” alisema Akilimali ambaye kwa mara ya kwanza alikuwa ameagizwa na uongozi wa Yanga azungumze na waandishi baada ya kuzuiwa katika mkutano mkuu uliopita wa wanachama wa klabu hiyo.
    “Tumebaini tunawekewa kauzibe katika kufanikisha suala hili zuri na baadhi ya viongozi waliochaguliwa na wananchi. Tunakipenda chama chetu cha CCM na Yanga ndiyo mwanzilishi wa chama hicho kwa sababu hata Mwenyekiti wa Kwanza wa TANU (Mwl. Julisu Nyerere) ndiye aliyekuwa mwanachama mwenye kadi nambari moja ya Yanga.
    “Kama wanaaumua kumwaga mboga, na sisi tutamwaga ugali 2014 na 2015 kwa sababu Yanga imekuwa ikisaidia sana CCM kufanya vizuri. Uwanja wetu utakuwa na faida kubwa kwa serikali ambayo itapata mapato. Tunashangaa kuwekewa kauzibe na viongozi wetu.
    “Tunawapa siku tano watupe jibu vinginevyo tutaomba kibali Jeshi la Polisi wanachama wa Yanga tuandamane dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye alifika hapa mwaka jana na kuagiza suala letu lishughulikiwe, au dhidi ya Mkuu wa Nchi kwa sababu watendaji wake wanakiuka Ilani ya Chama Tawala,” alisema zaidi Akilimali ambaye alikuwa amefuatana na viuongozi wengine wa Mabaraza la Wazee na Vijana wa Yanga.
    Mzee Akilimali ni mtu wa aina yake ndani ya Yanga SC na uongozi wa Manji umeweza kumtumia utakavyo na wakati mwingine umekuwa ukimtoa nishai vile vile.
    Jambo la kujiuliza hapa, ni juu ya ukweli halisi unaokwamisha uendelezaji wa Uwanja wa Kaunda, je ni kama ambavyo Wazee wa Yanga wanadai, au wanachama wa klabu hiyo wanapigwa changa la macho na viongozi wao? Jumapili njema. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAUKWA, PAKAWA YA UJENZI WA UWANJA WA KISASA YANGA SC, NI... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top