KIUNGO Mesut Ozil na timu yake ya taifa ya Ujerumani jana walizomewa na mashabiki wao mjini Stuttgart baada ya kuonyesha kiwango kibovu wakishinda bao 1-0 dhidi ya Chile katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Nyota huyo wa Arsenal alitolewa dakika ya 89 huku akizomewa na mashabiki wakaendelea kuzomea timu hadi mwisho wa mchezo.
Mario Gotze ndiye aliyeifungia bao pekee Ujerumani dakika ya 16 kwa pasi nzuri ya Ozil, lakini kwa ujumla mashabiki wa Ujerumani hawakuvutiwa na kiwango cha timu kuelekea Fainali za Kombe la Dunia katikati ya mwaka huu Brazil.
Lakini Ozil alitoa pasi ya bao pekee la ushindi la Ujerumani
0 comments:
Post a Comment