Na Dina Ismail, Dar es Salaam
MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Nteze John Lungu sasa amekuwa Mchungaji wa kanisa moja la kilokole nchini Marekani, imeelezwa.
Rafiki mmoja wa karibu Nteze, ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, Nteze aliyewika Pamba FC ya Mwanza na Simba SC ya Dar es Salaam, kwa sasa amekuwa mtumishi wa Mungu baada ya kustaafu soka.
Nteze aliibukia Pamba FC mwaka 1990 na mwaka 1994 akasajiliwa Simba SC hadi alipokwenda Afrika Kusini na Marekani kucheza soka ya kulipwa.
Nteze alirejea Simba SC mwaka 2002 na baada ya hapo akatungika daluga zake na kwenda kuishi Marekani.
Nteze ni kati ya wanasoka wachache waliopata mafanikio wakiwa na klabu na timu za taifa pia.
Kwani pamoja na kushinda mataji mawili ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, sasa Kombe la Kagame akiwa na Simba SC mwaka 1995 na 2002, pia alishinda Kombe la CECAFA Challenge mwaka 1994 akiwa na timu ya Bara, Kilimanjaro Stars nchini Kenya na Kombe la CECAFA Castle mwaka 2001 mjini Mwanza akiwa na Taifa Stars.

0 comments:
Post a Comment