Na Dina Ismail, Dar es Salaam
JUMA Abbas Pinto amefanikiwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) leo baada ya mpinzani wake George John Ishabairu kujitoa katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam.
George alitangaza kujitoa baada ya kufika ukumbini, akisema kwamba Mwajiri wake, Wizara ya Maji amemwambia ajitoe.
Pinto alipata kura 82 wakati 13 zilimkataa, na Egbert Mkoko ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 67 dhidi ya 32 za Mohammed Omary Masenga.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Wambura Mgoyo alimtaja Amir Mhando kushinda tena nafasi ya Ukatibu Mkuu baada ya kupata kura 93. Mhando hakuwa na mpinzani na kura mbili tu zilimkataa.
Nafasi ya Katibu Msaidizi imekwenda kwa Grace Aloyce Hoka aliyepata kura 65 dhidi ya 31 za Alfred Lucas Mapunda.
Mweka Hazina Msaidizi Zena Suleiman Chande amepata kura 55 dhidi ya 40 za Elius John Kambili, Mweka Hazina Shija Richard Shija 57 amepata kura 57 dhidi ya 38 za Mohamed Salim Mkangara.
Walioshinda nafasi za Ujumbe ni Ibrahim Mkomwa Bakari, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa na Urick Chacha Maginga.

Wanaume tumerudi; Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto kulia akipongezana na Katibu wake, Amir Mhando baada ya kutangazwa washindi mchana huu ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam. |
Kamati mpya ya Utendaji ya TASWA |
Hapa Pinto tu; Mmoja wa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TASWA, Mgaya Kingoba akipiga kura kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam leo. |
Pinto alipata kura 82 wakati 13 zilimkataa, na Egbert Mkoko ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kura 67 dhidi ya 32 za Mohammed Omary Masenga.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Wambura Mgoyo alimtaja Amir Mhando kushinda tena nafasi ya Ukatibu Mkuu baada ya kupata kura 93. Mhando hakuwa na mpinzani na kura mbili tu zilimkataa.
Nafasi ya Katibu Msaidizi imekwenda kwa Grace Aloyce Hoka aliyepata kura 65 dhidi ya 31 za Alfred Lucas Mapunda.
Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications, Frank Sanga akiwa amemshika mtoto Sheikh Yussuf Mahmoud Zubeiry wakati wa Mkutano wa TASWA leo |
Aliyeshindwa; Elizabeth Mayemba kulia aligombea Ujumbe akashindwa. Mwani Nyangassa wa pili ameshinda na kushoto ni mpiga kura Zaituni Kibwana |
Benny Kisaka kulia na Ibrahim Masoud 'Maestro' kushoto |
Sophia Asheri kulia na Somoe Ng'itu kushoto |
Mhariri wa magazeti ya mwishoni mwa wiki ya Habari Leo, Eric Anthony Mkuti kulia |
Dina Ismail alikuwepo |
Lehule Nyaulawa kulia akipongezana na Grace Hoka |
Mweka Hazina Msaidizi Zena Suleiman Chande amepata kura 55 dhidi ya 40 za Elius John Kambili, Mweka Hazina Shija Richard Shija 57 amepata kura 57 dhidi ya 38 za Mohamed Salim Mkangara.
Walioshinda nafasi za Ujumbe ni Ibrahim Mkomwa Bakari, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa na Urick Chacha Maginga.
0 comments:
Post a Comment