Na Renatus Mahima, Bagamoyo
MRISHO Ngassa amekwishaungana na timu yake, Yanga SC kambini katika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoani Pwani tayari kwa mchezo wa Jumatano dhidi ya Azam FC Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ ameondolewa kwenye programu ya mchezo huo.
Ngassa aliyekuwa mapumziko mjini Mwanza ameingia Kiromo leo na jioni hii ataanza mazoezi na wenzake, ingawa bado kucheza au kutocheza keshokutwa kutategemeana na hali yake.
Ngassa alitoka uwanjani kipindi cha pili Jumapili ya wiki iliyopita baada ya kuumia Yanga SC ikimenyana na Al Ahly ya Misri mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 1-1.
Na baada ya kutua Dar es Salaam Jumatano, alikwenda Mwanza mapumzikoni, huku wenzake wakiingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro Jumamosi iliyoisha kwa sare ya bila kufungana.
Kipa anayeonekana kuwa chaguo la kwanza Yanga chini ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm, Dida aliyedaka mechi zote dhidi ya Al Ahly na kupangua penalti mbili Uwanja wa Border Guard, aliumia mkono siku moja kabla ya mechi na Mtibwa na Juma Kaseja akaziba vyema pengo lake.
Wazi sasa Kaseja ndiye atakayepewa jukumu la kuzuia michomo ya Azam Jumatano. Mchezaji mwingine atakayekosekana kwenye mchezo wa keshokutwa ni majeruhi wa muda mrefu, kiungo Salum Telela.

Tegemeo Jangwani; Mrisho Ngassa kulia ameingia kambini Bagamoyo na jioni hii ataanza mazoezi na wenzake kujiandaa na mechi na Azam FC Jumatano |
Ngassa alitoka uwanjani kipindi cha pili Jumapili ya wiki iliyopita baada ya kuumia Yanga SC ikimenyana na Al Ahly ya Misri mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika na kutolewa kwa penalti 4-3 kufuatia sare ya jumla ya 1-1.
Na baada ya kutua Dar es Salaam Jumatano, alikwenda Mwanza mapumzikoni, huku wenzake wakiingia kambini kujiandaa na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar mjini Morogoro Jumamosi iliyoisha kwa sare ya bila kufungana.
Kipa anayeonekana kuwa chaguo la kwanza Yanga chini ya kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm, Dida aliyedaka mechi zote dhidi ya Al Ahly na kupangua penalti mbili Uwanja wa Border Guard, aliumia mkono siku moja kabla ya mechi na Mtibwa na Juma Kaseja akaziba vyema pengo lake.
Wazi sasa Kaseja ndiye atakayepewa jukumu la kuzuia michomo ya Azam Jumatano. Mchezaji mwingine atakayekosekana kwenye mchezo wa keshokutwa ni majeruhi wa muda mrefu, kiungo Salum Telela.
0 comments:
Post a Comment