MSHAMBULIAJI Neymar jana alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa Brazil wa 5-0 dhidi ya Afrika Kusini kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika kwenye Uwanja uliochezewa Fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010, Soccer City.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona sasa ametimiza jumla ya mabao 30 aliyoifungia Brazil, ambayo ilibadilisha jezi kipindi cha pili kutoka jezi zao za asili njano na nyeupe na kuvaa bluu tupu.
Neymar alifunga dakika za 41, 46 na 90 wakati mabao mengine ya Brazil yalifungwa na Oscar dakika ya 10 kabla ya Fernandinho dakika ya 79.
Neymar akimtungua kipa wa Afrika Kusini, Ronwan Williams kushoto
Neymar akishangilia bao lake la kwanza
0 comments:
Post a Comment