MSAKO wa Jose Mourinho wa mshambuliaji wa kiwango cha juu duniani unaelekea kufanikiwa kwa kuwa karibu kumnasa mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Diego Costa.
Chelsea ilimuangalia tena Jumatano ya jana wakati Atletico Madrid ilipoilaza Granada bao 1-0 katika La LIga, alilofunga mshambuliaji huyo na sasa ipo tayari kutoa Pauni Milioni 40 kumnunua mkali huyo wa mabao.
Costa, mwenye umri wa miaka 25, amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga mabao Hispania na amesaidia Atletico kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako itamenyana na Barcelona.
Atatua darajani? Chelsea iko mbioni kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania, Diego Costa anayechuana kwa mabao na Ronaldo na Messi La Liga |
Katika La Liga amefunga mabao 23 katika mechi 28, wakati Ligi ya Mabingwa amefunga mabao saba katika mechi tano- na kufanya jumla ya mabao 30 aliyofunga hadi sasa katika mechi 33.
Mazungumzo yanatarajiwa kuzaa matunda kutokana na Atletico kutaka kukamilisha usajili wa jumla wa kipa Thibaut Courtois, ambaye anacheza kwa mkopo kwao kutoka Stamford Bridge na Mourinho yuko tayari kuwaachia mlinda mlango huyo, ingawa alitarajiwa kuwa mrithi Petr Cech.
Kadhalika, badaka ya kumrejesha mshambuliaji wake Fernando Torres, klabu hiyo ya Hispania imeona bora kusajili wachezaji chipukizi kwa gharama nafuu.
0 comments:
Post a Comment